• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaongeza ufadhili kwa wanafunzi wa fani mbalimbali Tanzania kufikia 259 kwa mwaka

    (GMT+08:00) 2019-08-22 10:27:52

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    UFADHILI kutoka nchini China kwa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma fani mbalimbali nchini humo imeongezeka mara mbili zaidi mwaka huu kutoka wanafunzi 120 mpaka 259 mwaka jana .

    Hayo yamebainika wakati wa hafla maalum ya kuwaaga wanafunzi 61 wanaoenda nchini Chini ijayo kusomea fani mbalimbali ikiwemo 20 watakaosomea udaktari bingwa wa magonjwa ya figo na nyinginezo huku 41 wakisoma fani mbalimbali iliyofanyika katika ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.

    Waziri wa Elimu, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako anasema ufadhili wa masomo mbalimbali nchini humo umekuwa ukiongezeka kila wakati wakati mwaka huu wanafunzi watakaopata ufadhili toka serikali ya China na vyuo vikuu mbalimbali nchini humo wamefikia 259 mwaka huu toka 120 mwaka jana.

    Waziri anamuomba balozi wa China nchini Wang Ke kusaidia kuongeza ufadhili mpaka mara tatu ya sasa ili kupata wataalamu wa miradi ya kipaumbele kwa serikali ikiwemo wahandisi wa uendeshaji mradi wa umeme mkubwa wa Rufiji na undeshaji wa reli ya kisasa SGR.

    "Serikali inazidi kuomba ufadhili kwa wahandisi wa umeme mkubwa watakaosimamia mradi kuzalisha umeme wa Mwalimu Nyerere unaoendelea kujengwa katika bonde la mto rufiji pamoja na kufadhili wahandisi wa kuendesha mradi wa reli ya SGR"anasema Ndalichako.

    Anamshukuru balozi kwa kuonesha nia ya kuendelea kusaidia ufadhili kwa madaktari baada ya kupata ufadhili kwa wataalamu wa afya 20 kila mwaka baada ya Rais John Magufuli kumuomba Rais wa China Xi Jinping ufadhili huo mara baada ya kufika kwa meli ya matibabu nchini ikitokea China mwaka jana.

    Anasema baada kutokea kwa msongamano wa watu waliotaka matibabu kwa wataalamu hao toka china Rais Magufuli alimuandikia barua Rais Xi ambaye alikubali kuongeza ufadhili kwa wataalamu hao 20 kila mwaka kwa miaka mitatu hivyo Waziri Ndalichako ameomba kuongezwa idadi huku China wakifikilia kuendelea na ufadhili huo baada ya miaka mitatu waliyohaidi kwisha.

    Waziri anawaasa wanafunzi hao kutumia vema nafasi waliyopata kufadhiliwa na serikali na kuwa mabalozi wazuri ili kumaliza mafunzo hayo na kuwa wataalamu kwa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.

    Balozi Wang anasema mwaka huu wanafunzi 259 wanapata ufadhili toka nchini huo na mpaka sasa takribani China imetoa ufadhili kwa wanafunzi 1900 na programu za ufundi stadi kwa zaidi ya 6,100 kutokana na ushirikiano wa kihistoria wa nchi hizo mbili.

    Anasema wanafunzi wengi wa kitanzania wanachagua kusoma China kwa sasa wamedahili wanafunzi zaidi ya 5600 wanaosoma nchini humo ikiwemo 690 wanaofadhiliwa na serikali ya China wengine wakilipa wenyewe na wengine wakifadhiliwa na kada mbalimbali.

    Anasema mwaka huu nchi hiyo inatimiza miaka 55 tangu kuanza ushirikiano wa kidplomasia kati ya nchi hizo mbili huku wakishirikiana na kusaidiana katika nyanja mbalimbali na miaka ya hivi karibuni ushirikiano katika sekta ya elimu umekuwa mkubwa kwa serikali ya China ikitoa ufadhili katika elimu kila mwaka.

    Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana kulikuwa na wanafunzi wa kimataifa nchini China zaidi ya laki tano hivyo kuongoza kwa wanafunzi wa kigeni kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.

    inaelezwa kuwa vijana ni muelekeo wa nchi, hivyo ni matumaini vijana wanaoenda kusoma fani mbalimbali watatumia fursa hiyo kusoma kwa bidii ili kupata uelewa utakaosaidia maendeleo ya ujenzi wa nchi na watakaporejea nchini kuwa uti wa mgongo kwa uchumi na maendeleo ya jamii pamoja na Tanzania ya viwanda na hatimaye nchi kuwa ya uchumi wa kati.

    Naye Mwalikishi wa wanafunzi wanaoenda kusoma China, Dk Saria Kasianju alimuhakikishia waziri na balozi kuwa wataenda kuwakilisha vema nchi kwa kufuata taratibu na sheria za nchi hiyo hivyo kuwakilisha vema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako