• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kusaidia Afrika kupambana na Ebola na magonjwa mengine yanayoambukiza

    (GMT+08:00) 2019-08-29 10:03:50

    VICTOR ONYANGO

    BEIJING, CHINA

    China itaendelea kutoa msaada kwa nchi zenye shida za Ebola, Waziri Msaidizi wa China wa Mambo ya nje Chen Xiaodong alisema.

    Akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa nane wataalamu wa China-Africa Jumatatu mjini Beijing, bwana Chen alisema China ina wasiwasi kuhusu kuzuka kwa ebola kwenye nchi kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na serikali ya Rais Xi Jinping itajiunga na Afrika kuhakikisha kuwa janga la Ebola imemalizwa.

    "Tuliguswa na milipuko ya ebola barani Afrika na China itachukua hatua zote kuhakikisha kuwa Ebola inashughulikiwa, tutaongeza ushirikiano wetu na Afrika katika maeneo haya tunapoendelea kutoa misaada kwa maeneo yaliyoathirika," asema waziri Chen.

    Hii ni baada ya Shirika la Afya Duniani kutangaza kuzuka kwa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dharura ya afya ya umma ya wasiwasi wa kimataifa.

    Aliongeza kuwa China imechangia kwa kiasi kikubwa mapigano yanayoendelea barani Afrika dhidi ya kuzuka kwa Ebola na pia kwa maendeleo ya Kituo cha Afrika cha Kuzuia Magonjwa na Udhibiti.

    Mlipuko wa hivi karibuni wa virusi vya Ebola wa 10 huko DRC unaripotiwa kuwa milipuko la pili kubwa la Ebola, baada ya ile ya Afrika Magharibi mnamo 2015.

    Kufikia sasa, China ilikuwa nchi ya kwanza kutoa misaada kwa nchi zilizokumbwa na Ebola baada ya kuzuka kwa virusi vya Ebola mnamo Machi 2014.

    Mnamo Novemba 2014, China ilitoa misaada ya kibinadamu yenye thamani ya Yuan milioni 750 (karibu dola milioni 113.77) na ilipeleka maelfu ya wafanyikazi wa matibabu katika nchi zilizopigwa na Ebola katika raundi nne za kampeni.

    Kulingana na yeye, ushirikiano kati ya China na Afrika unaingia katika hatua mpya na matokeo mazuri yakifurahishwa na vyama vyote.

    "China iko tayari na imejitolea kusaidia Afrika kutatua shida zinazoikabili bara hilo pamoja na mambo yanayohusiana na afya na haya yote yanawezekana kupitia ushirikiano mpana, "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako