• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vijana 20 Tanzania wajiunga na sanaa ya Wing Chun toka China

  (GMT+08:00) 2019-08-30 17:13:13

  Na Theopista Nsanzugwanko, Dar es salaam

  VIJANA 20 kutoka eneo la Murieti jijini Arusha wamejiunga katika Sanaa mpya ya mapigano iliyoanzishwa ijulikanayo Kama 'Wing Chun'.

  Mwanzilishi na mkufunzi was Sanaa hiyo Rashid Said amesema kuwa ni mchezo mpya umeingia kwa Kasi nchini kutokana na vijana kuuelewa haraka.

  Alisema asili ya Wing Chun ni nchini China na unaendelea kusambaa maeneo mbalimbali ni miongoni mwa michezo ambayo inafundishwa kihalali na umesashasajiliwa.

  "Mchezo huu unasaidia kutengeneza nidhamu nzuri katika jamii pia ulinzi binafsi hivyo ukiwa na Mazoezi ya mchezo huo utakupa ulinzi katika kukabiliana na changamoto kadhaa," anasema Said.

  Anabainisha kuwa malengo ni kuwatengeneza vijana wake katika maadali yanayostahili pia kutengeneza ajira na kuwaepusha kujihusisha na tabia hatarishi ambazo hazifai katika jamii nzima.

  Naye Mkurugenzi wa shirikisho la West coast Shotokan Karate Association ambaye pia Ni Mwenyekiti wa Karate mkoa Arusha Sensei Daddy Kassim alisema mchezo huo kwa Tanzania ni moja ya mchezo unaokuja kwa Kasi na utasaidia kukuza michezo hiyo ya Sanaa ya mapigano Kanda ya kaskazini na kusema vijana hao waliouanzisha wataweza kuendesha Jambo hilo kwa utimilifu.

  Sensei Kassim alisema katika kukuza Sanaa ya mapigano kutakuwa na semina itakayowakutanisha washiriki kutoka michezo yofauti na itafanyika mwezi wa Septemba ili kuwawezehsa vijana kupata mafunzo na vyeti vya kimataifa vitakavyowapa uwezo wa kufundisha na itaendesha na mkufunzi kutoka Mauritius.

  "Tunaendelea kufanya juhudi kuhakikisha vijana wetu wanaweza kupata ujuzi mpya kutoka hatua Moja kwenda nyingine ili kuiweka Sanaa ya mapigano iwe katika mfumo wa ajira na tunashukuru mapka sasa baadhi ya wanamichezo wameshapata ajira katika ngazi mbalimbali,"alisema Sensei.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako