• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya imezindua kituo cha kukuza utamaduni, biashara na utalii mjini Beijing ili kuvutia wachina wengi kutembelea Kenya

  (GMT+08:00) 2019-08-30 17:21:49
  NA VICTOR ONYANGO

  BEIJING, CHINA

  Katika harakati za kuimarisha uhusiano baina ya Kenya na China, Balozi wa Kenya huko Beijing Sarah Serem leo amezindua kituo cha kukuza utamaduni na kibiashara ikiwemo utalii ijulikanayo kama CCCPK.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, balozi Serem alisema kwamba ya CCCPK ni ushuhuda wa uhusiano unaokua wa watu na watu kati ya nchi hizo mbili na kuongeza kuwa watu wa China wanakaribishwa kutembelea Kenya kama watalii na pia wawekezaji.

  "Kenya na China zina historia ndefu ya kushirikiana katika nyanja zote za maisha ikiwa ni pamoja na kisiasa, kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kwa watu kubadilishana. Kwa sasa, tuna kampuni nyingi za kichina zimeweka maduka nchini Kenya na ziliboresha uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili. Tunapozindua CCCPK, ningependa kuwaalika mashirika zaidi ya wachina kuwekeza Kenya kwa sababu wataweza kupata soko la Afrika Mashariki vizuri," bi Serem aeleza.

  Alisema kuwa bidhaa za utalii za Kenya ni baadhi ya zilizoandaliwa vizuri barani Afrika na ulimwenguni na kuna miundombinu ya kiwango cha dunia kukaribisha mamilioni ya watalii wapo pamoja na mbuga zilizohifadhiwa, za wanyama wa porini zilizohifadhiwa na Kenya kwa ubinadamu mzuri kwa watalii wa China kujionea.

  Kenya ilihesabu wageni wa China wapatao 82,000 mnamo 2018, ongezeko la asilimia 37.7 ikilinganishwa na mwaka uliopita, kulingana na data ya serikali ya Kenya. Lakini, nchi hiyo ya Afrika Mashariki inatarajia kuvutia watalii wa karibu milioni moja wa Kichina kila mwaka.

  Bi Serem aliongezea kuwa "ni kwa msingi huu madhubuti kuwa Balozi wa Jamhuri ya Kenya huko Beijing ataanzisha CCCPK nchini China kwa lengo la kukuza zaidi Kenya kwa idadi ya Wachina na kuhimiza harakati za watu, bidhaa na huduma."

  Balozi wa zamani wa China nchini Kenya kati ya 2003 na 2006 Guo Chongli, aliipongeza Kenya kwa kuwa ndio ufafanuzi wa kweli wa ushirikiano kamili wa China na Africa.

  "Uhusiano mkubwa tunaona sasa kati ya nchi hizi mbili ni ufafanuzi wa kweli wa ushirikiano mpya wa wa faida pande zote. Inaweza kupatikana nyuma wakati wa nasaba ya Ming wakati Kenya ilipeana twiga kwa China ambayo Mfalme aliitunza kwenye Palace mueseum na wakati rais wa Kenya wa zamani Mwai Kibaki alitembelea China aliulizia. Chenye tunaona kwa sasa ni tajriba mkuu wa rais wa sasa Uhuru Kenyatta ambaye baada ya kuchaguliwa, amefanya mengi kwa kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili," bwana Guo asema.

  CCCPK itafanya kikamilifu na kwa dhati ubadilishanaji wa ushirikiano na ushirikiano kati ya Kenya na serikali za mitaa na wafanyabiashara nchini China chini ya mfumo wa Ukanda mmoja, Njia moja.

  Itatoa njia bora ya ushirikiano wa kitamaduni na biashara ili kuimarisha ushirikiano zaidi wa vitendo katika biashara, uchumi, utamaduni na utalii. Itasaidia makampuni ya wachina kuelewa soko la Kenya bora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako