• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya Kimataifa ya Hongwei toka China yaajiri vijana 514 kuchakata mazao ya misitu Mufindi

  (GMT+08:00) 2019-08-30 17:24:06
  Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

  VIJANA 514 kati yao wanawake 310 wamenufaika na uwekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Hongwei toka nchini China kwa kujipatia ajira za kudumu na za muda kupitia kiwanda chake cha kuchakata mazao ya misitu kilichojengwa mjini Mafinga, wilayani Mufindi.

  Kiasi kinachokadiriwa kufikia Dola za Kimarekeni Milioni 4 (sawa za na zaidi ya Sh Bilioni 8) zimewekezwa katika kiwanda hicho kinachotengeneza Marine Board, Plywood na block board zinazotumika kwa shughuli mbalimbali za ujenzi.

  Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Zheng Xi aliwaambia waandishi wa habari kuridhishwa na kasi ya Rais Dk John Magufuli kuwakaribisha wawekezaji kwa kuwa Uchumi wa viwanda nchini Tanzania unazidi kuimarika na idadi ya raia wa China a wenye shauku ya kuwekeza inaongezeka

  Zhengi Xi anasema kwa kupitia kampuni yao kuna wawekezaji wengine kutoka China ambao hivikaribuni walikutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi katika mchakato wao wa kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza karatasi katika wilaya hiyo hiyo ya Mufindi inayoongoza kwa uzalishaji wa miti ya kupandwa nchini.

  "Tunampongeza sana Rais Dk John Magufuli kwa kutengeneza sera rafiki za uwekezaji Tanzania. Tangu tuwekeze kiwanda hiki miaka mitatu iliyopita, tumekuwa tukilipa kodi ya wastani wa Sh Bilioni 1 kwa mwaka, kiasi ambacho tunaamini kina mchango kwa maendeleo ya Taifa," alisema

  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William anazidi kuwaalika wawekezaji kutoka nchini China na maeneo mbalimbali kuwekeza katika wilaya hiyo kutokana na mazingira mazuri waliyowawekea huku wakiwa karibu nao katika masuala mbalimbali

  "Wawekezaji toka nje ni sehemu ya maendeleo ya watanzania na Taifa kwa ujumla kwani uwekezaji wao unatengeneza masoko ya malighafi zetu, ajira na ni moja ya chanzo cha mapato ya wananchi na Taifa."Anasema

  Anabainisha kuwa hadi mwisho wa mwaka wa fedha 2018/2019, wilaya ya Mufindi ilikuwa na jumla ya viwanda vikubwa, vya kati na vidogo 161 katika mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu, ambavyo kwa pamoja vimeajiri watu zaidi ya 10,000.

  Alikipongeza kiwanda cha Hongwei kwa kinazingatia taratibu, kanuni na sheria za nchi, na ni walipaji wazuri wa kodi serikalini hivyo ni lazima kilindwe kama vinavyolindwa viwanda vingine na shughuli zingine za kiuchumi.

  "Hivikaribuni kumetokea mambo yanayohukihusisha kiwanda hiki na tuhuma mbalimbali. Tumeyapokea kwa masikitiko makubwa kwasababu uchunguzi wa Polisi unaonesha ni ya kupikwa na kuna baadhi ya vyama vya siasa vinatumika kujipatia mtaji wa kisiasa," anasema.

  Anatoa onyo kwa baadhi ya vyama vya siasa (hakuvitaja) vinapita kwenye viwanda hivyo, kuwarubuni vijana na kujaribu kufanya maeneo hayo ya uzalishaji kuwa vijiwe vya siasa na propaganda jambo lisilokubalika kwa jamii.

  Walikanusha kufanyiwa vitendo vya ukatili, baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho walisema toka wapate ajira kiwandani hapa, hali ya maisha yao inazidi kubadilika.

  Wakati Ayubu Peter (24) kutoka Mwanza anasema kiwanda hicho kimemuwezesha kumudu maisha yake ya kila siku huku Furaha Mbembati (25) na Grace Mgina (27) wameweza kununua mashamba na wanalea watoto wao vizuri.

  Pamoja na kuchangia shughuli za maendeleo ya jamii inayowazunguka, Afisa muajiri wa kiwanda hicho, Michael Mkamba anasema kiwanda chao kipo katika mchakato wa kupanua shughuli zake, mpango utakaokwenda sambamba na kuboresha mazingira ya kazi ya wafanyakazi wake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako