• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pato la kigeni la Kenya kuongezeka baada ya nchi hiyo kufanya makubaliano na China kuhusu chai ya zambarau

    (GMT+08:00) 2019-09-06 10:20:03

    Na Eric Biegon, NAIROBI

    China imefungua milango yake kwa bidhaa zaidi za kilimo kutoka Kenya. Kuanzia sasa kwenda mbele, wakulima wa chai ya rangi ya zambarau katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki wataanza kusafirisha chai maalumu kwa soko la China baada ya makampuni mawili kutoka nchi hiyo ya bara Asia kufanya makubaliano ya kutangaza mpango wa kusambaza zao hilo nchini China.

    Wizara ya kilimo Mwangi Kiunjuri inaamini kwamba mpango wa kuuza nje chai maalum ya Kenya kwenda China italetea taifa hilo pato zaidi la fedha za kigeni.

    Makumpuni ya hiyo ya Benny na Zhegzhou Two Straits Enterprise pia yanapanga kupanua uzalishaji wa chai ya rangi ya zambarau nchini Kenya hadi kilo 5,000,000 kila mwaka katika miaka mitatu ijayo ili kukidhi mahitaji.

    "Hamu hii ilitokana na utambuzi kwamba China ni mnunuzi anayeongoza wa chai kutoka nje, huku Kenya ni mzalishaji mashuhuri wa chai ya ubora wa juu." Waziri wa kilimo alibainisha

    Kwa miaka mingi, Kenya imekuwa miongoni mwa mataifa makubwa wazalishaji wa majani ya chai, hii ikiwa ni pamoja na hesabu ya chai nyeusi kwa asilimia 90 ya mauzo ya jumla ya chai.

    Hata hivyo, karibuni, kilimo cha chai kisicho cha kawaida kimekuwa kikipata umaarufu miongoni mwa wakulima hasa kutokana na mahitaji makubwa ya chai ya kijani na zambarau katika soko la kimataifa.

    China ni nchi ya hivi karibuni kuonyesha nia kutaka chai ya zambarau ya Kenya baada ya kampuni ya chai ya Benny na Zhengzhou two Straits Enterprise na serikali kurahisisha usafirishaji wa chai hiyo spesheli hadi China.

    "Kampuni za China zina uhakika kwamba watazinunua kila aina ya chai zinazozalishwa kupitia mpango huu na kuwekwa kwa meli tayari kusafirishwa kuelekea China." Waziri Kiunjuri alisema.

    Kwa mujibu wa Zhu Zhonghai, ambaye aliongoza ujumbe huo uliozuru Nairobi, China bado ni soko muhimu sana kwa ajili ya kukuza bidhaa za majani ya rangi ya zambarau na maalum isiyo ya kawaida.

    "China pia ni mnunuzi mkuu wa aina ya chai ya CTC kutokana na ongezeko la mahitaji ya wanunuzi wa Kichina katika kuweka ushirikiano wa kimkakati na wazalishaji wa chai wa Kenya," alisema.

    Chini ya mpango huo, makampuni haya mawili pia yataanzisha programu ya kuongeza uzalishaji wa chai ya rangi ya zambarau kutoka kilo 1,000,000 sasa kwa mwaka, hadi kilo 5,000,000 kila mwaka katika miaka mitatu ijayo na kilo 30,000,000 katika miaka 10 ijayo ili kukidhi mahitaji ya chai hiyo China.

    "China kwa sasa ni mwagizaji wa chai nyeusi ya CTC, chai ya papo hapo na nyingine maalum kutoka India, Sri Lanka na Kenya," alisema.

    Serikali ya Kenya imedokeza kuwa itaongeza mapato yatokanayo na chai maalumu kwa mwaka hadi bilioni 7 kwa miaka mitano na shilingi bilioni 40 kwa miaka kati ya 5 na 10 ijayo.

    Aidha, viwanda vitatu maalum vya chai kutoka Kenya vitafaidika kutokana na vifaa muhimu vya teknologia ya kisasa katika jitihada za kuongeza uzalishaji wa chai hiyo ya rangi ya zambarau.

    Kampuni hizo mbili pia zitatoa huduma za hifadhi kwa kampuni yoyote ya Kenya itakayoanza kuuza chai yake nchini China.

    Zhonghai alisema kwa kipindi cha miaka saba iliyopita, China imekuwa ikisafirisha chai kila mara kutoka mataifa mengine ili kutimiza mahitaji yanayotokana na watumiaji wa chai katika maeneo ya mijini nchini China ambao wamekuza ladha ya chaii aina ya CTC.

    Na ili kukidhi mahitaji yanayohitajika ya chai hii maalumu, Kiunjuri amefichua kwamba makampuni haya mawili ya China yatatoa mashine za uzalishaji wa majani chai na utaalamu wa kiufundi kwa angalau viwanda vitano vya chai nchini Kenya.

    Aidha mwenyekiti wa Two-straits Enterprise Management Company Zhang Hongchao alitoa msaada wa dola 150,000 kufadhili sekta ya elimu ndani ya sehemu ya kuzalisha chai nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako