• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chuo Kikuu cha Nairobi imefanya makubaliano na China kujenga kituo cha uhamishaji wa teknolojia ya kilimo

  (GMT+08:00) 2019-09-09 14:07:47

  NA VICTOR ONYANGO

  BEIJING, CHINA

  Chuo Kikuu cha Nairobi siku ya jumamosi iliingia katika makubaliano na mkoa wa China ya Ningxia ili kujenga kitengo cha uhamishaji wa kilimo na teknolojia ya China na Arabuni.

  Makubaliano hayo yalitiwa saini kati ya Profesa Stephen Kiama kaimu naibu wa chansela wa rasilimali watu ambaye pia ni mkuu wa kitivo cha kilimo cha chuo kikuu cha Nairobi, Minghong Yang, naibu mkurugenzi wa idara ya kilimo na maswala ya mkoa wa Ningxia na Anthony Gicharu mshauri mkuu wa kimkakati wa kampuni ya Cherami Africa wakati wa maonyesho ya biashara ya nne kati ya China na nchi za kiarabu.

  Kituo hicho kitatumika kukuza watu zaidi kubadilishana wa watu kwa watu katika uwanja wa kilimo na teknolojia kwa kushughulikia maswala ya usalama wa chakula nchini Kenya na nchi za Kiarabu.

  Akizungumza baada ya sherehe ya utiaji saini, Profesa Kiama alisisitiza kwamba taasisi za masomo ya juu zina jukumu muhimu katika mfumo wa ushirikiano kati ya nchi kwani kituo hicho kitakuza sana katika uhusiano wa China na Waarabu tu bali pia na Kenya-China pia.

  Profesa Kiama aliongezea kuwa kwa sasa Kenya inazingatia usalama wa chakula na kituo hicho kikianza kufanya kazi kitakuwa muhimu kwa taasisi hiyo mbali kwamba watakuwa na utafiti mwingi unaozunguka uwanja wa kilimo na teknolojia na jinsi zinaweza kusaidia kufanikisha ajenda ya nchi hiyo katika suala la uzalishaji wa chakula.

  "Kukamilika kwake, tutahakikisha tunapata suluhisho zaidi kuhusu ushirikiano wa kilimo," asema Profesa Kiama.

  Kwa upande wake, bwana Minghong alisema kuwa kituo hicho kitazingatia kukuza teknolojia juu ya ufugaji wa kuku wa kawaida na uzuiaji na udhibiti wa magonjwa ya kuku.

  "Kwa madhumuni ya utofauti, tunapenda kituo cha Kenya kuzingatia kuku na magonjwa yanayohusiana nayo ingawa utafiti mwingine mwingi utafanywa pia," aeleza bwana Minghong.

  Huu umefanyika baada ya vituo vya uhamasishaji vya teknolojia ya kilimo nje ya nchi kuwa tayari vimeanzishwa na Ningxia huko Mauritania, Kyrgyzstan na Jordan kwa miaka kadhaa kufuatia kuzinduliwa kwa Kituo cha Uhamisho wa Teknolojia ya kilimo cha China na Arabuni mnamo 2015.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako