• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UDSM yajivunia uhusiano Tanzania na China kuleta manufaa ya kielimu

    (GMT+08:00) 2019-09-16 10:27:59

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimejivunia manufaa ya kielimu waliyopata kutokana na wahadhili na wanafunzi wake kwenda kusoma nchini China katika fani mblimbali.

    Wameeleza hiyo imetokana na uhusiano mzuri kati ya China na Tanzania uliosaidia kuwezesha wahadhiri na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kubadilishana uzoefu katika elimu.

    Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye anasema hayo wakati akizindua warsha iliyoandaliwa na chuo hicho kupitia Taasisi ya Confucius pamoja na idara ya Historia, kuhusu ushirikiano wa China na Tanzania.

    Anasema kupitia ushirikiano huo wa kihistoria kwa nchi hizi, China imekuwa ikitoa nafasi kwa wahadhiri na wanafunzi wa UDSM kwenda kusoma kwenye vyuo vyao katika fani mbalimbali.

    "Tuna uhusiano katika masuala ya historia, hapa chuoni kuna kituo cha historia cha kimataifa. Mahala popote kunapokuwa na mabadilishano ya mawazo kwa wanafunzi wanapata vitu vipya katika kibadilishana ujuzi," anasema Profesa Anangisye.

    Mkurugenzi katika Taasisi ya Confucius chuoni hapo, Profesa Aldian Mutembei anasema idara ya historia ya UDSM imeandaa majadiliano yatakayoelezea maendeleo yaliyopo.

    "China kwa sasa imepiga hatua kubwa katika maendeleo inabidi kuangalia ni wapi kama Tanzania tulikosea ili kuwa sawa kwani miaka ya sitini nchi hizi mbili zilikuwa sawa kiuchumi," anasema.

    Anasema majadiliano mengine yatalenga uhusiano wa vyama vya siasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Cha cha Kikomunisti China, vijana, uchumi pamoja na biashara katika nchi hizo mbili.

    Anasema vijana wa China wameelimishwa na kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa tofauti na wa Tanzania ambako wengi wao wanasubiri ajira ambazo ni chache.

    "Kuna kundi kubwa la vijana wangependa kujiajiri, ni namna gani vijana wa China walivyoelimishwa na kutoa mawazo ya kuajiriwa mpaka kujiajiri," anasema Profesa Mutembei.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa China, Gao Wei anasema mwaka huu Tanzania na China inasheherekea miaka 55 ya uhusiano. Kwa mujibu wa Gao, mpaka sasa nchi yake imetoa nafasi za masomo kwa watanzania 1,700.

    Anasema pia China imetoa wataalamu wake katika fani za udaktari, jeshi na kilimo kusaidia maendeleo ya taifa na kuimarisha maisha ya Watanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako