• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi China lamkabidhi Rais Magufuli magari 40 ya JWTZ

    (GMT+08:00) 2019-09-16 10:28:20

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    JESHI la Ukombozi wa watu wa China (PLA) limekabidhi Jeshi la Ulinzi la wananachi wa Tanzania (JWTZ) magari 40.

    Magari hayo yamepokelewa na Rais John Magufuli ambaye amemshukuru Rais wa Jamahuri ya watu wa China Xi Jinping kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano mzuri wa Tanzania na China ikiwemo misaada ya uekezaji ambayo China inaufanya hapa.

    Alisema pamoja na kusaidia serikali katika maeneo mbalimbali ya huduma za jamii, ulinzi na usalama ,na miundombinu, China ndiyonchi inayoongeza kwa uwekezaji nchini ikiwa na miradi 723 yenye thamani ya shilingi Trilioni 13.581 na iliyozalisha ajira 87,126.

    Ametaka uhusiano huo uimarishwe zaidi kwa JWTZ na PLA kujenga kiwanda kikubwa chenye uwezo wa kubangua tani laki mbili za korosho kwa mwaka ,jambo litakalosaidia kuongeza thamani ya korosho kwa mwaka huku ikiongeza thamani ya jeshi kwa wakulima na kupeleka China kwenye mahitaji ya Korosho.

    Amemuomba balozi wa China nchini, Wang Ke na Kanali Shao Yuanming aliyeiwakilisha PLA katika makabidhianoya magari hayo kufikisha shukrani zake kwa Rais Xi Jinping kwa kuendeleza na kukuza uhusiano na ushirikiano baina ya China na Tanzania na ujengwa kwa kiwanda.

    Ameshukuru China kwa kutoa msaada wa magari hayo ambayo amesema yataimarisha utendaji kazi wa jeshi hilo na kuomba PLA isaidie upatikanaji wa ndege kubwa kubebea askari na vifaa kwaajili ya jeshi hilo .

    Alisema makabidhiano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano wa karibu,kindugu na kirafiki kati ya mataifa haya mawili, tunashukuru China kwa misaada mbalimbali na mwaka huu Tanzania inatarajia kupokea watalii 10,000 kutoka China.

    Luteni Yuanming ameshukuru Rais Magufuli kuudhuria hafla hiyo,ili kuendeleza na kukuza uhusiano wan chi hizo ikiwemo uhusiano wa kijeshi na kuhaidi kuwa PLA itaendelea kushirikiana kwaukaribu na JWTZ.

    hukuMkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen Venance Mabeyo ametaja maeneo ambayo jeshi hilo limenufaika kwa ushirikiano huo kuwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha mafunzo ya kijeshi huko Mapinga Bagamoyo kilichoharimu Sh. Bilioni 137.63, ujenzi wa awamu ya pili wa chuo cha ulinzi wa Taifa jijini Dar es Salaam utakaogharimu bilioni 57.

    Alisema kwa sasa PLA inaamilisha maandalizi ya kujenga makao makuu ya JWTZ Dodoma na kushirikiana na JWTZ katika zoezi kubwa la kijeshi litakalofanyika nchini kwa lengo la kubadilishana ujuzi katikaulinzi na usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako