• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kwenye mpango wa Mkanda Mmoja Njia Moja

  (GMT+08:00) 2019-09-18 08:55:33

  Na Eric Biegon - BEIJING

  Kongamano la jukwaa la mtandao wa habari la Mkanda Mmoja Njia Moja maarufu kama Belt and Road News Network (BRNN) lilingoa nanga katika mji mkuu wa China, Beijing, tarehe 16 Septemba, 2019, na kuwavutia waandishi wa habari 50 wanaowakilisha vyombo vya habari maarufu 46 kutoka nchi 26 mbalimbali kutoka bara Afrika na Amerika ya Kusini.

  Wakati wa sherehe za ufunguzi, serikali ya China ilizungumzia jukumu kubwa la vyombo vya habari hasa wakati ambapo utekelezaji wa miradi chini ya mpango wa Mkanda Mmoja Njia Moja unapochukua sura mpya.

  Kwa mujibu wa naibu mkuu wa idara ya utangazaji ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Jiang Jianguo, kwa kutoa taarifa za habari sahihi, za kweli na za kina kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kijamii miongoni mwa mataifa yaliyotia saini kwenye mpango huo, waandishi wa habari watakuwa nguzo muhimu ya uwezeshaji wa mpango huo.

  Jiang anasisitiza kuwa mpango wa Mkanda Mmoja Njia Moja ni mfumo wa ushirikiano wa kimataifa ambao unalenga tu kufaidi mataifa na watu hasa katika nchi zinazoendelea duniani.

  "Itakuwa vyema kwa wataalamu na wanahabari kwenye vyombo vya habari, kupitia BRNN, waunde jukwaa la ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama na kusaidia kuanzisha taratibu za uendeshaji ambazo zitaimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa mradi." Alisema

  Kwa mujibu wa mhariri mkuu wa gazeti la People's Daily Tuo Zhen, wanaoshiriki kongamano hilo watabadilishana mawazo kuhusu jinsi gani itasaidia kuimarisha ushirikiano wa vyombo vya habari katika jitihada za kutimiza malengo ya jukwaa hilo la BRNN kama vile kuimarisha ufahamu wa watu ambayo ni kipengele muhimu cha mpango wowote wa maendeleo.

  Hata hivyo, Tuo alielezea wasiwasi wake kuhusu baadhi ya vyombo vya habari ambazo kwa maoni yake yanajaribu kila kuchao kupaka tope mpango huo licha ya maendeleo ya hali ya juu yanayodhihirika katika nchi ambako miradi chini ya Mkanda Mmoja Njia Moja yanatekelezwa.

  "Tunataka kutumia jukwaa hili kueneza ufahamu mahsusi na unaofaa kuhusu mpango wa Mkanda Mmoja Njia Moja. Jukwaa hili linakusudia kukuza mawasiliano kati ya Mataifa na tamaduni mbalimbali wakati ambapo inawezesha ushirikiano katika sekta mbalimbali baina ya nchi." Alisema

  Jukwaa hilo lililoundwa kwa ushirikiano wa ofisi ya baraza la nchi ya China, Idara ya uhusiano wa nje ya gazeti la People's Daily na Chuo Kikuu cha mawasiliano cha China, CUC, inatazamiwa kusaidia katika kurejesha utamaduni wa uwazi, na kuheshimiana baina ya mataifa kwa ajili ya mafanikio ya mpango huo .

  Katika moyo wa mkanda huu wa Silk, mkuu wa Chuo Kikuu cha mawasiliano cha China Liao Xiangzhong alibainisha kuwa mpango huo umeandikisha mafanikio makubwa katika miaka sita yaliyopita, kama inavyoshuhudiwa kutokana na mapokezi mema ambayo BRI imepata kutoka kwa mataifa mengi.

  Bwana Liao alifichua kuwa ujenzi wa taasisi ya utafiti katika Chuo Kikuu hicho unaendelea huku akisema taasisi hiyo itakuwa ikichunguza njia za kuhakikisha mpango huo utakuwa mkubwa zaidi katika karne hii.

  "Tunapaswa kuzikumbatia faida za kipekee zitokanazo na vyombo vya habari katika mawasiliano hili tujenge jukwaa la manufaa." Alisisitiza.

  Alihoji kuwa hii ndio ndoto ya Rais wa China Xi Jinping ya kutaka kuboresha mfumo wa utawala wa kiuchumi wa kimataifa, kukuza maendeleo ya kawaida na kujenga jamii yenye kujali mustakabali wa raia wote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako