• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar yaahidi kuimarisha ushirikiano na China National Research Institute of Food & Fermentation Industries

    (GMT+08:00) 2019-10-08 09:50:35

    Na Majaliwa Christopher

    SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitiza kuwa itazidi kupanua wigo wa ushirikiano kati yake na China National Research Institute of Food & Fermentation Industries katika suala la upatikanaji wa mafunzo kwa watendaji wake kupitia sekta tofauti.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, alitoa msisitizo huo jana Jumatatu, Oktoba 7, 2019, alipozungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Dong Jianhui Ofisini kwake visiwani humo.

    Wakufunzi kutoka Taasisi hiyo ya China wapo Zanzibar wakiendelea na utoaji wa mafunzo ya ya Upishi na Ukarimu kwa watendaji wanaotowa huduma kwa Viongozi wakuu wa Serikali pamoja na sekta binafsi.

    Mafunzo hayo yaliodumu kwa takriban wiki tatu na yalitarajiwa kuhitimishwa Oktoba 08, mwaka huu.

    Alisema Serikali itaendeleza ushirikiano kwa kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na uongozi wa taasisi hiyo katika utoaji wa mafunzo ya Upishi na ukarimu kwa mwaka wa tatu hivi sasa, pamoja na kaungalia uwezekano wa kuyafikia maeneo mengine.

    Alisema ushirikiano huo utaimarika kikamilifu pale Serikali itakapofanikisha hatua za kutuliana saini makubaliano ya awali (memorandum of understanding) kati yake na taasisi hiyo.

    Aidha, aliipongeza Wizara inayosimamia upatikanaji wa mafunzo ya nchini China kwa kuunga mkono utoaji wa mafunzo hayo kwa mwaka wa tatu mfululizo, hivyo kuleta mabadiliko makubwa na kuinua uwezo wa watendaji nchini.

    Salum, alieleza matumzini yake ya kiongozi huyo kukutana na viongozi wa Idara ya Maendeleo ya Utalii, iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA pamoja na Wakala wa Chakula, dawa na Vipodozi ili kuweza kubadilishana uzoefu na utaalamu katika kipindi atakachokuwepo nchini.

    Nae, Mkurugenzi Mkuu kutoka taasisi ya China National Reseach Insitute of Food & Fermentation Industries Dong Jianhui alisema taasisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo ya upishi na ukarimu kwa watendaji mbalimbali, ikiwa ni hatua ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano kati yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

    Aliipongeza Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa juhudi zake na kuunga mkono na kufanikisha utoaji wa mafunzo hayo.

    Aidha, Mkurugenzi huyo alisifia mandhari nzuri ya Zanzibar pamoja na usalama wa kutosha uliopo hapa nchini.

    Katika hatua nyengine, kiongozi huyo alikutana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) na Wakala wa Chakula, Dawa an Vipodozi na kuahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano kati ya taasisi hizo kwa mustakbali mwema na maendeleo ya Zanzibar.

    Dong alisema katika maeneo mbali mbali aliyotembelea ikiwemo la uzalishaji wa viungo Kizimbani, amebaini Zanzibar kuwa na utajiri mkubwa bidhaa za chakula, lakini kilichokosekana ni utaalamu wa kusarifu bidhaa hizo, hivyo alibainisha azma ya Taasisi hiyo kusaidia utaalamu ili kuziongea thamani bidhaa hizo na kuleta tija katika soko la Utalii.

    Aidha Mkurugenzi huyo alitembelea Ofisi za Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi zilizopo Mombasa na kukutana na uongozi wa Wakala huo, ambapo uongozi wa taaasisi hiyo umeomba msaada wa kuwajengea uwezo watendaji wake kwa kuwapatia mafunzo ili waweze kutekeleza vyema majukumu yao.

    Mkurigenzi Mtendaji wa Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Dk. Burhan Othman alisema kuna umuhimu kwa watendaji wa Ofisi kupatiwa fursa za mafunzo yatakayowajengea uwezo, hususan katika suala la ukaguzi wa chakula.

    Nae, Mkurugenzi Taasisi ya Utalii Zanzibar, iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA, Dk. Aley Soud aliiomba taasisi hiyo kuzingatia mahitaji yaliopo kwa kubadilishana na uzoefu na fursa za mafunzo kwa watendaji wa taasisi hiyo, ikiwa ni hatua ya kuongeza ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili.

    Alisema wakati huu Zanzibar ikiimarisha uchumi wake kupitia sekta ya utalii kumekuwepo na ongezeko kubwa la Watalii kutoka China wanaozuru nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako