• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa wito wa ushirikiano zaidi wa vyombo vya habari kutoka nchi zinazoendelea

  (GMT+08:00) 2019-10-08 09:53:26

  NA VICTOR ONYANGO

  BEIJING, CHINA

  China imewahimiza waandishi wa habari wa Kiafrika, Asia, Pasifiki na Amerika ya Kusini kuwa wawe wakiripoti ukweli bila upendeleo kuhusu kuelezea hadithi za China kwa ulimwengu.

  Akihutubia waandishi wa habari kutoka mataifa yanayoendelea Jumapili mjini Beijing, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje, Hua Chunying alisema kuwa vyombo vya habari vina jukumu muhimu katika uhusiano wa China na nchi zingine.

  "China imepiga hatua kubwa katika maendeleo yake katika miongo saba kwa mfano, kuinua milioni 850 kutoka kwa umaskini na ni vyombo vya habari ambavyo vinaweza kuripoti hii kwa usahihi bila kushawishiwa na vyombo vya habari vya magharibi," asema bi Hua.

  Ata hivyo, bi Hua aliongezea kuwa ulimwengu unakabiliwa na changamoto kadhaa kwa sasa kama nchi zinazoendelea zinanyanyaswa na nchi zilizoendelea lakini hayo yanaweza piti ikiwa waandishi wetu wa habari wataripoti mambo jinsi wanavyotokea.

  Maoni yake yalichangiwa na rais wa Chama cha Wanadiplomasia wa Umma wa China Wu Hailong, chama ambacho kimekuwa kikiwafundisha waandishi wa habari kutoka Afrika, Asia, Pasifiki na Amerika ya Kusini kwa miezi 10 kila mwaka nchini China tangu 2014, kwamba jamii bora inaweza kujengwa tu ikiwa waandishi wa habari wataripoti maswala na usawa.

  Aliongeza kuwa China inabaki kuwa taifa kubwa zaidi ulimwenguni kwa sasa na iko tayari kushiriki maendeleo yake na nchi zingine za ulimwengu wa tatu na ili hii ifanikiwe, vyombo vya habari vinabaki vyombo jukumu muhimu kwa watu kubadilishana na kwa hivyo kuna haja ya kuwa na ushirikiano zaidi wa waandishi kati ya nchi hizo na Beijing.

  "Waandishi wa habari wanahitaji kukuza ushirikiano wao kwa madhumuni ya kujenga jamii yenye nia ya pamoja. Sisi ni watu walio na umilele sawa na hatupaswi kuruhusu watu wengine kutupotosha," asema bwana Wu.

  Bwana Wu alieleza kuwa "diplomasia ya China ni moja ambayo hainyanyasi nchi yoyote na Rais Xi Jinping anaona umuhimu mkubwa kwa ushirikiano wa faida na ndio maana waandishi wetu wanahitaji kufanya."

  Balozi wa zamani wa China nchini Moroko Cheng Tao kwa upande wake alisisitiza juu ya haja ya mipango zaidi ya kubadilishana kati ya waandishi wa habari wa China na wale kutoka nchi zinazoendelea kuelewana kila mmoja kwa madhumuni ya kushiriki hadithi za China kwa wazi.

  "Nyinyi nyote mnatoka katika nchi wanachama wa BRI na mmeona aina ya maendeleo ambayo China inafanya katika nchi zenu, ulimwengu unahitaji kujua hii na ili iwezekane, tunahitaji kuona waandishi wetu wa habari wakijihusisha na mipango ya kubadilishana ili tusiwe na upotoshaji katika kuripoti, ushirikiano huu unategemea waandishi wa habari," asema bwana Cheng.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako