• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya waandishi 120 kutoka nchi mbali mbali wakutana Zhejiang, China kujadili njia za ushirikiano

    (GMT+08:00) 2019-10-14 09:40:03

    VICTOR ONYANGO

    HANGZHOU, ZHEJIANG

    Mkoa wa Kusini mashariki mwa China, Zhejiang Ijumaa ilizindua mkutano wa kwanza wa ushirikiano wa wanahabari na mawasiliano na miji ya kimataifa kwa lengo la kuelezea hadithi za China kwa Ulimwengu.

    Mkutano huo uliwavutia waandishi wa habari zaidi ya 120 kutoka nchi 67, kutoka Afrika, Amerika ya Kusini, Urusi, Ulaya, China na Japan.

    Kilichotokea katika mkutano huo ni mwito wa waandishi wa habari kuimarisha ushirikiano wao wakati huu ambao ulimwengu unakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo mabadiliko ya hali ya hewa.

    Akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi mjini Hangzhou, Zhu Guoxian, mjumbe wa kamati ya kudumu ya CPC Kamati ya Mkoa ya Zhejiang, alisisitiza kwamba vyombo vya habari vina umuhimu mkubwa katika kuleta watu wa kila aina pamoja kwa hivyo wanahitaji kufanya jukumu lao kwa ufanisi.

    "China inazingatia umuhimu mkubwa kwa watu hadi kwa watu kubadilishana na ili hii ipatikane, vyombo vya habari vinapaswa kuongeza ushirikiano wao na kuuambia ulimwengu nini kinajumuisha, " asema bw Zhu.

    Aliongezea kuwa vyombo vya habari vinachangia pakubwa kwenye uhusiano wa Beijing na ulimwengu.

    Balozi wa zamani wa Afrika kusini nchini China bw Gert Grobler alitoa changamoto kwa waandishi kuripoti ukweli bila ubaguzi wowote.

    Kwa madhumuni ya kuongeza kuelewana kati ya Zhejiang na kampuni za vyombo vya habari nje ya nchi, washiriki kadhaa walitoa hotuba kuu katika mkutano huo kufafanua juu ya biashara za ulimwengu na kuweka mbele mapendekezo ya kuwezesha ushirikiano wa pande zote.

    Hafla hii inadhaminiwa na Ofisi ya Habari ya Serikali ya Watu wa Mkoa wa Zhejiang na Idara ya Mambo ya nje ya Zhejiang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako