• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakabidhi jengo la Dola Milion 22 kwa Serikali ya Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-10-15 09:36:36

    Na Majaliwa Christopher

    SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China imekabidhi jengo jipya lenye gharama ya Dola za Kimarekani Milioni 22 (sawa na Shilingi Bilioni 50 za Tanzania) kwa Serikali ya Tanzania.

    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Prof Palamagamba Kabudi na maofisa wengine kutoka Serikalini walipokea jengo hilo ambalo litatumiwa na wizara hiyo ya mambo ya nje.

    Jengo hilo lililoko katikati ya jiji la Dar es Salaam ni la ghorofa sita --na ni muendelezo wa jitihada za nchi hiyo ya Asia ya Mashariki kusaidia na kushirikiana na Tanzania katika harakati zake za maendeleo hasa katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki inalenga uchumi wa Viwanda.

    "Ni heshima kubwa kupata msaada wa namna hii kutoka kwa wenzetu wa China, hii ni ushuhuda mwingine wa namna hizi nchi mbili zinavyozidi kuimarisha uhusiano na urafiki wao uliodumu kwa miongo mingi iliyopita," alisema Prof Kabudi katika hafla ya kupokea jengo hilo siku ya Jumatano, Oktoba 9, 2019.

    Waziri Kabudi alieleza kuwa urafiki wa China na Tanzania ni wa muda wote na ni wa kweli na mfano bora wa kuigwa.

    Waziri huyo aliongeza kuwa kukamilika kwa jengo na hatimaye kukabadhiwa kwa Serikali ya Tanzania kumekuja kipindi ambacho taifa hilo la Asia ya Mashariki, linaadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake pamoja na kumbukumbu ya miaka 55 ya uhusiano wa China na Tanzania.

    Kwa upande wake, Balozi Wang alisema kuwa jengo hilo linakabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania kipindi ambacho nchi hiyo imechukua uenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

    Balozi Wang alisema kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha malengo yake ya mendeleo ya kiuchumi yanafikiwa, akisisitiza kuwa kupitia kwa Jukwa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) nchi hizo mbili zimenuia kuimarisha ushirikiano wao.

    Jengo hilo lililokabidhiwa jijini Dar es Salaam na Balozi Wang limejengwa na kampuni ya China Anhui Foreign Economic Construction (Group) Co. Ltd. Ujenzi wa mradi mradi huo ulianza mwezi Agosti, 2016.

    "Leo tuna furahi kukabidhi jengo hili kwa Serikali ya Tanzania. Ni jengo lililofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na pia limejengwa na kampuni kutoka nchini China" alisema Bi. Wang mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Prof Palamagamba Kabudi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako