• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Antonio Gutteres apongeza juhudi za China za kupiga umaskini teke

  (GMT+08:00) 2019-10-17 14:30:40

  NA VICTOR ONYANGO

  BEIJING, CHINA

  Bosi wa Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Antonio Gutteres amepongeza China kwa bidii yake ya kuondoa watu millioni 700 kwenye umaskini kwa muda wa miongo nne.

  Kupitia kwa ujumbe wake maalum uliosomwa na mratibu mkazi wa UN nchini China Bw. Nicholas Rosellini siku ya Alhamisi mjini Beijing wakati wa kongamano wa kupunguza umaskini duniani, Katibu mkuu wa UN alihimiza nchi zinazoendelea kujifunza kupitia uzoefu wa China kupunguza umaskini.

  "Takriban watu millioni 700 wametolewa kwenye umaskini na serikali ya China ndani ya kipindi cha miongo nne, kitu ambacho nchi zinazoekumbwa na umaskini zinaezajifunza na kufuata nyayo za Beijing. Wakifanya hivyo, watachangia pakuu katika malengo ya maendeleo endelevu, "asema Bw. Gutteres.

  Alisema kuwa sera ya China ya kufungua soko lake kwa ulimwengu umechangia pakuu kukabiliana na changamoto ya umaskini na kusisitiza kuwa China lazima iendelee na mipango ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu anajipata kwenye umaskini wakati China itakuwa imepunguza umaskini kabisa mwaka ujao.

  "Baada ya kufikia lengo la umaskini sifuri mwaka ujao, uendelevu wa upunguzaji wa umasikini unabaki kuwa muhimu hapa, kila mtu lazima aletwe kwenye bodi ili kuchangia kwenye Pato la Taifa. Kutoa huduma bora kwa wananchi ni lazima," asisitiza Bw Gutteres.

  Bw. Gutteres aliongekuwa kuwa kuna haja ya kushirikiana ili kukabiliana na umaskini ili kutoa malezi bora kwa watoto kwa sababu umaskini unanyima watoto wengi haki yao ya maisha bora.

  "Kila nchi lazima ihakikishe kuwa watoto wamelindwa vizuri hata kama umaskini na ongezeko la joto duniani huleta tishio kubwa kwao," Bw Gutteres asema.

  Kwa upande wake, naibu waziri mkuu wa China Bw. Hu Chunhua alisema kuwa China itaendelea kukabiliana na janga la umaskini kwa sababu nchi inathamini ustawi wa watu wake na ile ya washirika wake.

  Alifichua kuwa nchi hiyo imefanikiwa pakuu kupunguza umaskini kupitia mwokozo wa Chama cha Kikomunisti cha China na Rais Xi Jinping akiwa msingi wa kati.

  "Chama yetu chini ya mwokozo wa Rais Xi imepiga hatua kuu kukabiliana na umaskini. Mnamo 2015, Rais Xi alitoa wito wa kila mtu kujitahidi ili kumaliza umaskini na hii ilifanya umaskini kupungua na asimilia 87 kulingana na viwango vya Benki ya Dunia ya dola 1.9 kwa siku," asema Bw Hu.

  Alisema kuwa tangu 2012 hadi 2018, umaskini umepungua kutoka watu millioni 98 hadi millioni 16 na wanatarajia nambari hizo kufika sifuri.

  Bw. Hu alieleza kuwa China iko tayari kila mara kubadilishana uzoefu wake wa kupiga umaskini teke na nchi zote duniani akihimiza kuwa kuna nia ya kushirikiana ili kujenga jamii na shauku ya pamoja kwa wanadamu.

  Kulingana na waziri wa Jumuiya ya Ujumuishaji na Uwezeshaji Uchumi wa Morisi Bw. Marie Roland, hakuna nchi inaezamaliza umaskini bila sera nzuri kama zinazowezesha China kupiga umaskini teke na ushirikiano wa faida za upande zote, kwa hivyo, kuna haja za nchi kufanya kazi pamoja ili kumaliza umaskini ulimwenguni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako