• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kuanza kutoa filamu pamoja na StarTimes

  (GMT+08:00) 2019-11-07 14:40:49

  NA VICTOR ONYANGO

  Kampuni ya StarTimes ya China itafanya utengenezaji wa filamu inayolenga kufunua Kenya kwa kina kwa wachina ili wafahamu zaidi.

  Rais wa StarTimes bwana Pang Xinxing alihakikishia balozi wa Kenya nchini China Bibi Sarah Serem siku ya Jumatano kuwa kampuni hiyo iko tayari kuanza utengenezaji wa filamu pamoja na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia.

  "StarTimes iko tayari kufanya kazi pamoja na Kenya ili kutoa filamu yenye maudhui ya nchi hiyo, " asema bwana Pang.

  Kampuni itatumia teknolojia yake na wakurungezi wa filamu wenye tajriba kuu na umarufu zaidi ilikusaidia filamu za Kenya kupata soko nchini China.

  Msingi wa utengenezaji wa filamu pamoja ni kuboresha ushirikiano baina nchi hizo mbili ili kuhakikisha uhusiano huo umefikia watu wote hadi mashinani.

  "Tukifanya kazi pamoja, filamu hizo zitapea wachina kutoka sehemu mbalimbali kufahamu historia na utamaduni wa Kenya na hivyo basi kuchangia pakuu katika sekta ya utalii nchini Kenya," aongezea bwana Pang.

  Kwa upande wake, balozi Serem alisema kuwa amedhamiria kuwa utengenezaji wa filamu za asili za wakenya zitabadilisha tasnia ya filamu nchini na hata kuunda fursa zaidi za kazi na pia kufanya wachina wengi kuelewa nchi inayotembelea.

  Aliongeza kuwa StarTimes katika soko la Kenya ni kielelezo cha kweli cha dhamana kubwa kati ya Nairobi na Beijing kwa hivyo ni wakati wa watu zaidi kubadilishana na kukuza talanta mbalimbali miongoni mwa wakenya.

  "Ofisi yangu iko tayari kuwezesha kitu chochote kinachohitajika ili kuhakikisha kuwa mradi huu unafanikiwa na kufikia wakenya na wachina pamoja," bi Serem asema.

  Hii ni baada ya Tume ya Filamu ya Kenya wiki jana kusaini mkataba wa kuelewana na kampuni ya televisheni ya dijitali StarTimes kuunda ushirikiano wa kimkakati kabla ya toleo la 9 la tuzo za filamu za kimataifa za Kalasha na Televisheni tukio la kila mwaka na tume ambayo inasherehekea talanta ya kipekee katika filamu na runinga.

  Akiongea wakati wa hafla ya utiaji saini wa MOU, Bwana Timothy Owase - Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Filamu Kenya alibaini kuwa, "Kama Tume, tunakaribisha uwekezaji kama huu na sekta binafsi kwenye tasnia. Hii itakuza tasnia ya utazamaji nchini, kuwapa watengenezaji wa sinema na kufanya utengenezaji wa sinema kuwa mradi mzuri. Ushirikiano huo unafungua soko kubwa kwa watengenezaji wa sinema za ndani kuonyesha vipaji vyao na jukwaa pia kuhakikisha kwamba yaliyomo yetu yanaweza kupita katika mipaka yetu na hivyo kutoa athari kubwa katika mkoa. "

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako