• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawapa wanakijiji mbegu kompyuta

    (GMT+08:00) 2019-11-11 09:34:56

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    BALOZI wa China nchini Tanzania Bibi Wang Ke amekabidhi msaada wa mbegu za Alizeti, Choroko na Mahindi zenye uzito wa kilo 4800 ambazo zitagaiwa kwa wananchi wa kijiji Mhenda kilicho jirani na Hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro.

    Lengo ni kuwawezesha wanakijiji hususan vijana kujielekeza kwenye kilimo na kuachana na vitendo vya ujangili na uwindaji haramu wa wanyamapori.

    Alisema kuwa sekta ya utalii imekuwa ikichangia pato la taifa kwa asilimia 17.6 hivyo lazima wananchi waache vitendo vya ujangili ili hifadhi ziwe na wanyamapori wa kutosha watakaowavutia watalii kutokana na kwamba kilimo cha kisasa na chenye tija ndio kinachoweza kuongeza kipato kwa wananchi wanaozunguka hifadhi na sio vitendo vya ujangili na uwidhaji haramu.

    Balozi Wang anasema kuwa mbali ya kutoa msaada wa mbegu pia ametoa msaada wa kompyuta mpakato nne na runinga kubwa kwa ajili ya uongozi wa hifadhi ya Taifa Mikumi pamoja na sare kwa ajili ya askari wa polisi jamii wa kijiji cha Kisaki.

    Anasema kuwa mwaka jana watalii kutoka China walifikia 34,000 hivyo aliwataka wananchi kulinda hifadhi hiyo pamoja na wanyama ili kukuza utalii utaonufaisha Taifa na kwamba China imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kukuza utalii.

    Aidha anasema kuwa mwaka jana China kupitia mabadiliko mbalimbali ya sheria ilitunga sheria ya kudhibiti na kukataza uwindaji haramu.

    Aidha, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Costantine Kanyasu amewataka wananchi wa kijiji hicho kuacha uwindaji haramu wa wanyama unaosababisha wanyama pori kutoweka.

    Naibu waziri huyo anasema kuwa kwa mwaka huu watalii wakiwemo wa kutoka China watakaokwenda kwenye maeneo mbalimbali ya hifadhi wanarajia kufikia 1.7 milioni hivyo lazima maeneo ya hifadhi yalindwe ili wanyama waongezeke.

    Anasema kuwa zamani China ilikuwa ndio soko kubwa na pembe za ndovu lakini hivi sasa China wametunga sheria kukomesha biashara hiyo, hivyo na sisi watanzania lazima tutafute shughuli nyingine za kufanya ikiwemo Kilimo badala ya kutegemea ujangili ambao kwa sasa haulipi.

    Naye,.mkurugenzi wa taasisi ya kupambana na majanga na maafa ya Sukos Kova, Kamishina mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova anasema kuwa uwindaji haramu katika hifadhi ya Mikumi unafanywa na baadhi ya wananchi wakiwemo vijana kutokana na kukosa kazi za kuwaingizia vipato.

    Anabainisha kuwa taasisi hiyo iliamua kushirikiana na serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii pamoja na ubalozi wa China kuhakikisha wananchi wa kijiji cha Mhenda ambacho kipo jirani na hifadhi wanapewa msaada wa mbegu bora ili waweze kupata kipato kupitia kilimo chenye tija.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako