• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wanafunzi wanaosoma Kichina Chuo Kikuu Cha Dodoma yaongezeka

    (GMT+08:00) 2019-11-22 16:21:50

    Na Majaliwa Christopher

    IDADI ya wanafunzi wanaosoma lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Dodoma imeongezeka kutoka mwanafunzi mmoja mwaka 2016 kozi hiyo ilipoanzsishwa hadi kufikia zaidi ya 100 mwezi Novemba, mwaka huu, 2019.

    Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius katika Chuo hicho Dkt. Yang Lung aliambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa namba ya wanafunzi wanaojitokeza kuchukua kozi ya somo hilo imekuwa ikiongezeka kila mwaka, akiongeza kuwa mwaka jana, 2018, chuo hicho kilisajili jumla ya wanafunzi 97 kwa ajili ya programu hiyo.

    "Mahitaji ya lugha ya Kichina chuoni hapa yanazidi kuongezeka. Hadi wakati huu, zaidi ya wanafunzi 100 wanasomea programu hii," alisema mkurugenzi huyo, akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa wanafunzi 20 kutoka Huazhong University of Science and Technology.

    Wanfunzi hao kutoka China, wanatembelea Taasisi za Confucius katika nchi tatu za Afrika --Tanzania, Botswana na Comoro.

    Dkt. Yang alisema kwamba pamoja na kutembelea nchi hizo tatu za Afrika katika Taasisi za Confucius kubadilisha uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali, wanalenga pia kueneza utamaduni wa China katika nchi hizo.

    Aliongeza kuwa pia kuna mpango wa kuanzisha Taasisi ya Confucius katika Chuo Cha Mtakatifu John kilichopo Dodoma ikiwa na lengo la kuongeza wigo wa wanafunzi wengi kusomea programu hiyo ya Kichina.

    Dkt. Yang alisema kuwa kikwazo kikubwa katika urafiki kati ya China na Tanzania kilikuwa ni uelewa mdogo wa Kichina na kwamba, fursa zinazotokana na kuielewa lugha hiyo ni nyingi sana ndani na nje ya nchi.

    Aliongeza kuwa Watanzania wakiilewa lugha ya Kichina na utamaduni wa nchi hiyo watakuwa na nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika kupata manufaa yanayotokana na ukubwa wa uchumi wa China.

    Alisisitiza kuwa wananchi wa Tanzania wanastahili kuitumia ipasavyo taasisi inayofundisha masuala ya China ili kujiongezea maarifa kutokana na ukweli kuwa uchumi wa China unazidi kukua na Tanzania ina nafasi kunufaika.

    Mmoja wa wanafunzi wanaosomea programu hiyo ya lugha ya Kichina katika Chuo Cha Dodoma, Zakia Juma alisema aliamua kusomea kozi hiyo ili kupanua uelewa wake katika lugha nyingi za kimataifa.

    "Ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kichina...lugha hii itanipa fursa ya kujua mambo mengi yanayoendelea duniani ukizungatia kuwa China ni nchi iliyopiga hatua kubwa sana kimaendeleo," alisema Zakia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako