• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Madaktari bingwa wa moyo kutoka Fuwai Hospital-China kuwasili Tanzania

  (GMT+08:00) 2019-11-26 09:45:06

  Na Majaliwa Christopher

  USHIRIKIANO wa China na Tanzania katika sekta ya afya unazidi kuimarika siku baada ya siku huku timu ya madaktari bingwa wa Moyo kutoka Fuwai Hospital ya nchini China wakitarajiwa kuwasili katika nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki Novemba 28, mwaka huu 2019.

  Taarifa iliyotolewa jana, Jumamosi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, nchini Tanzania, ilieleza kuwa timu hiyo ya madaktari bingwa itakuwa nchini humo hadi Novemba 30, 2019.

  Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano katika wizara hiyo Bw. Emanuel Buhohela, ilieleza kuwa timu hiyo ya madaktari bingwa itaungana na wenzao wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

  Wakiwa nchini Tanzania katika Taasisi hiyi ya JKCIA, madaktari hao watafanya upasuaji kwa wagonjwa--ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa wakati wa ziara ya Waziri wa Afya Bi. Ummy Mwalimu nchini China iliyofanyika mwezi Agosti 2019.

  Hospitali ya Moyo ya Fuwai inaongoza ulimwenguni katika taasisi za matibabu ya Moyo ikiwa na vitanda 1200.

  Kupitia ushirikiano wa hospitali hiyo na JKCI- wataalam mabingwa wa Moyo kutoka JKCI wameanza kupata mafunzo katika hospitali ya Fuwai.

  Programu hiyo inajumuisha mafunzo ya teknolojia iliyovumbuliwa na Daktari Bingwa Prof PAN ijulikanayo kama (Percutaneous and Non-fluoroscopical procedure) ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za upasuaji wa moyo. Habari Picha kwa hisani ya Mdau Phelisters Wegesa-Beijing China.

  China na Tanzania zilianza ushirikiano katika sekta ya Afya tangu mwaka 1968, ambapo madaktari kutoka nchi hiyo ya Asia ya Mashariki wamekuwa wakitembela Tanzania katika mikoa mbalimbali kutoa huduma za afya.

  Hadi mwaka jana, mataifa hayo mawili walipoadhimisha miaka 50 ya ushirikiano katika sekta hiyo, takwimu zilionyesha kuwa zaid ya madaktari bingwa 1,200 kutoka China walishatembelea Tanzania kwa ajili ya kusaidiana na kuwajengea uwezo zaidi madaktari wa Tanzania.

  Ushirikiano huo pia umeisadia Tanzania kujenga Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete,ikiwa ni taaisi ya moyo kubwa ndani ya Afrika Mashariki.

  Tangu kuanza kwa ushirikiano huo, nchi hiyo ya Asia ya Mashariki imeendelea kuleta Madaktari wakujitolea katika Hospitali mbalimbali zilizopo nchini Tanzania zikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na JKCI.

  Vilevile hatua ya China kusaidia ujenzi wa Taasisi ya JKCI, imesaidia kuokoa gharama za kusafirisha wagonjwa kwenda kutibiwa nje ambapo takwimu zinaonyesha kuwa wagonjwa 85 kati ya 100 walikuwa wanatibiwa nje ambapo kwa sasa wagonjwa 85 wanatibiwa hapa nchini na 15 ndio hupelekwa nje ya nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako