• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vyombo vya habari vimehimizwa kujenga ulimwengu wa umoja

  (GMT+08:00) 2019-12-04 13:52:47

  NA VICTOR ONYANGO

  BEIJING, CHINA

  Waandishi wa habari kote ulimwenguni wamehimizwa kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa dunia kupitia hadithi zao.

  Akiongea wakati wa Mkutano wa Vyombo vya Habari ulioandaliwa na mjini Beijing Jumatano, Rais wa China Media Group (CMG) Shen Haixiong alisema kuwa uchumi wa dunia unapitia mabadiliko makubwa na yanakabiliwa na tishio la ulinzi kwa hivyo vyombo vya habari vinahitaji kujenga nguvu kupitia ripoti zao.

  "Pamoja na ulinzi katika kutokuwa na uhakika huu katika uchumi wa ulimwengu, vyombo vya habari vinahitaji kuwa vya kujenga na sio uharibifu," asema bwana Shen.

  Aliongezea kuwa vyombo vya habari vinahitaji kusaidia katika kujenga jamii na mustakabali wa pamoja wa wanadamu.

  Kwa upande wake, mwenyekiti wa Taasisi ya Ubunifu na Mkakati wa China bwana Zheng Bijian, alisema kuwa kuna haja ya kuelewa changamoto zinazokumba dunia kwa sasa, kwa hivyo, wanahabari wanafaa kuelimisha watu kuhusu haya changamoto na kutaja suluhisho bila ubaguzi wowote.

  Alisisitiza kuwa kuelewa ulimwengu imekuwa jambo muhimu kwa wakati huu, ni kupitia mabadiliko tofauti tunapopata utandawazi wa uchumi, kwa wakati huu, nchi zingine kubwa zinajaribu kupinga harakati hii kwa kuwanyanyasa wengine kwa ulinzi wao.

  "Ni muhimu kwa vyombo vya habari kuchukua jukumu lake katika utawala wa ulimwengu ambao utakuwa na faida kwa wote," asisitiza bwana Zheng.

  Aliongezea kuwa: "tunahitaji kujihusisha, sio kutengana na utandawazi na Uchina itaendelea kufanya kazi na nchi zingine kufanikisha hii nchi zinazoendelea zaidi."

  Waziri Mkuu mstaafu wa Ubelgiji Elio Di Rupo alipongeza China kwa kuchangia pakuu katika maendeleo endelevu (SDGs) wa Umoja wa Mataifa (UN).

  Bwana Rupo alisema kuwa juhudi za China za kupiga umaskani teke ufikapo mwaka wa 2020 zinaingiliana na malengo ya Umoja wa Mataifa.

  "China imechangia sana kupitia juhudi za kupunguza umasikini zilizoshuhudiwa, inaendelea kuchangia ustawi wa ulimwengu kupitia kujenga jamii iliyo na siku za usoni, mabadiliko ya hali ya hewa, Ukanda mmoja, Njia moja miongoni mwa wengine, " asema Bw Rupo.

  Alihimiza nchi kuzingatia njia ya mazungumzo katika kushughulikia mabadiliko ya kimataifa na kuheshima maoni ya kila mmoja katika utawala wa kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako