• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtanzania ashinda tuzo China kwa kubuni chakula cha samaki cha gharama nafuu

    (GMT+08:00) 2019-12-10 08:51:59

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    MWANAFUNZI wa Kitanzania Amos Benjamin aliyepata ufadhili toka serikali ya China mwaka 2017 na kuhitimu Chuo Kikuu cha Kilimo China mwezi uliopita ametunukiwa tuzo kutokana na ubunifu wa teknolojia ya ufugaji samaki maarufu "2019 UNLEASH Award for Innovative Fish Farming Technology" katika Shindano lililofanyika Shenzhen China.

    Shindano hilo la ubunifu duniani linawakutanisha wabunifu 1,000 duniani ni maalum kutafuta suluhisho ili kufikia lengo la maendeleo endelevu la Umoja wa mataifa .

    Amos anaamini kuwa kusoma kwake China kumemwezesha kupata ujuzi wa uliomsaidia kutunukiwa tuzo hiyo yenye lengo la kubadilisha jamii katika kuondokana na umasikini.

    Anaeleza kuwa akiwa nchini China alipata fursa ya kutembelea majimbo mbalimbali kuangalia mchango wa sekta ya kilimo kwa maendeleo ya China.

    "Nimejikita katika kuangalia mchango wa ufugaji samaki katika kuondoa umasikini kwa jamii masikini China, nilijifunza mengi na kufungua ufahamu wangu kwa jinsi ufugaji wa samaki ulivyo fursa katika usalama wa chakula na maendeleo ya uchumi nchini"anasema.

    Anabainisha kuwa kwa wafugaji samaki, jamii masikini zinaweza kukabiliana na changamoto katika ufugaji kwani ni gharama kubwa za uzalishaji ikiambatana na chakula cha samaki.

    "Ndiyo sababu niliamua kufanya utafiti kutafuta kwa jinsi gani China imefanikiwa katika ufugaji samaki na kwa nini chakula cha samaki China kinapatikana kwa urahisi kuliko nchini Tanzania" anasema.

    Pia, anasema ana rafiki yake aliyepata shahada ya uzamili nchini Indonesia ambaye alimhamasisha kufanya utafiti kama huo nchini Indonesia na kutokana na tafiti hizo ikanilazimu kutafuta chakula muafaka na ndiyo sababu ya kupatikana na NovFeed.

    Lengo letu ni kuzalisha chakula cha gharama nafuu na ubora madhubuti iliyotengenezwa kwa mmea aina ya magugu maji na funza ambayo ni nafuu kwa asilimia 30 kuliko chakula cha samaki kinachouzwa madukani.

    Anasema wanafahamu kuwa matokeo ya kazi hiyo itahamaisha sekta ya ufugaji samaki na kusaidia utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa taifa unaolenga kujenga uchumi wa viwanda.

    Mwezi uliopita kuangalia matokeo ya utafiti wao kwa kupeleka katika shindano hilo na waliwasilisha wazo lao kati ya washiriki 1,000 kutoka nchi 143 na kusimamiwa na wataalamu wa wanyama na chakula cha samaki toka China, huku wengine wakitumika katika fursa za mradi katika biashara na matokeo

    Baada ya uchunguzi wa wataalamu NovFeed ilitangazwa kuwa na mradi bunifu, endelevu na fursa kubadilisha maisha ya watanzania wengi pamoja na duniani.

    Anaishukuru Wizara ya biashara China kwa kutoa msaada wa kifedha na Chuo Kikuu cha Kilimo China elimu na mukaribu wao wakati wa masomo yake china.

    Anasema China iko tayari kusaidia katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kutaka vijana zaidi kujitokeza kuomba ufadhili na kutaka serikali ya Tanzania kutumia fursa zilizotolewa katika mkutano wa FOCAC uliofanyika Beijing Septemba 2018.

    China iko tayari kuanzisha karakana kumi kutoa elimu ya mafunzo ya ufundi kwa vijana hivyo kuomba wazungumze na China kupata Karakana moja

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako