• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yathibitisha kuwa ni mshirika wa karibu wa Kenya kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi

  (GMT+08:00) 2019-12-23 09:35:58

  Na Eric Biegon – NAIROBI

  Mwezi mmoja uliopita, kaunti ya Pokot Magharibi iliyoko katika mkoa wa Bonde la Ufa nchini Kenya iligonga vichwa vya habari baada ya kukumbwa na mkasa wa maporomoko ya ardhi. Janga hili lilisababishwa na mvua kubwa iliyokuwa ikushuhidiwa katika sehemu hiyo.
  Kutokana na mkasa huo, zaidi ya watu 50 walipoteza maisha yao, makumi ya maelfu wengine wakiachwa bila makazi, mali kuharibiwa na sehemu kubwa ya miundombinu kuharibiwa kabisa.
  Katika uharibifu huo wa kihistoria, idadi kubwa ya vijiji vilikuwa vimetengwa  na sehemu nyingine nchini, na kuweka maisha ya idadi kubwa ya wenyeji hatarini. 
  Huu bila shaka, ulikuwa wakati wa dhiki kwa wenyeji na Wakenya kwa ujumla. Lakini wakati hofu kiliongezeka kuhusu uwezekano wa kutokea janga la kibinadamu usio na kifani, taasisi moja lilijitokeza.
  Jumuiya ya makampuni kutoka China zinazohudumu nchini Kenya maarufu kama KCETA, ilikuwa ya kwanza kuchukua hatua kutokana na mkasa huo. Jumuiya hii ilikuwa miongoni mwa taasisi za kwanza kabisa kuwahi kufika katika eneo la mkasa ili kutoa msaada kwa walioathirika kwa maporomoko hayo ya ardhi.
  Siku moja tu baada ya maporomoko hayo kuripotiwa, taasisi hiyo ilihamasisha wanachama wake kuanzisha mchakato wa kuwasaidia wale walioathiriwa kutokana na mvua nyingi iliyokuwa ikinyesha.
  Mwenyekiti wa KCETA Li Changgui alibainisha kuwa Jamii ya biashara ya China nchini Kenya ilichukua hatua hiyo kwa sababu iliguzwa na madhara yaliyotokana na mkasa huo ambao ulichochewa na mvua kubwa.
  Wanachama wa jumuiya hiyo baadaye walitekeleza jukumu muhimu katika juhudi za uopoaji katika maeneo yaliyokubwa na janga hilo.
  Muda mfupi baada ya kuchipuka kwa habari hizo, kampuni moja ya ujenzi ya China ilielekea kwa haraka katika eneo hilo. Kampuni hiyo ilitwikwa jukumu la kurejesha miundombinu ya usafirishaji na kufungua barabara ambazo zilikuwa zimeharibiwa na mvua ili kuwezesha serikali na mashirika mengine ya kibinadamu kama vile ule wa Msalaba Mwekundu kupeleka msaada uliohitajika sana kwa walioathirika.
  Kampuni ya Kichina ya STECOL CORPORATION, hasa iliwatuma wafanyakazi wake na vifaa vya kwa ujenzi katika eneo hilo kufanya marekebisho ya dharura ya barabara zilizoharibiwa. Kwa muda mfupi, sehemu ya barabara iliyoathiriwa ilikuwa imetengenezwa na kufunguliwa.
  Maporomoko hayo yalikuwa makubwa na yalizuia barabara, na kufunga eneo hilo pasipo sehemu ya kupenyeza. Kutokana na hali hii, vikosi vya uokoaji kwa kiasi kikubwa vilikosa kufika eneo hilo kwa muda unaofaa.
  Ni wazi kwamba janga hilo liligusa taifa la China. Katika ujumbe wake wa salamu za rambirambi na huruma kwa Rais Uhuru Kenyatta, Rais wa China Xi Jinping alibainisha kwamba alishtushwa kusikia kuhusu mkasa huo wa maporomoko ya ardhi katika Kaunti ya Pokot Magharibi, ambayo ilisababisha madhara makubwa.
   "Kwa niaba ya serikali ya China na watu wa China, na kwa niaba yangu mwenyewe, ningependa kutoa maombolezo yangu kwa wahanga na kuonyesha huruma kwa majeruhi na familia zilizofiwa. " Rais Xi alisema.
  Chini ya uongozi wa ubalozi wa China nchini Kenya, KCETA ilianza kupeleka bidhaa vya dharura vya kula na visivyo vyakula kwa waathiriwa. Tani nyingi za vifaa vya msaada, ikiwa ni pamoja na vyakula, bidhaa za watoto, bidhaa za kike, blanketi, miongoni mwa mengine, zilisafirishwa kwa mamia ya familia ambazo zilikuwa zimelazimishwa kukaa kwenye kambi zilizoandaliwa kwa ajili ya waathiriwa.
  Balozi wa China nchini Kenya bwana Wu Peng alizisifu makampuni ya China kwa michango yao, na kueleza kwamba juhudi zao nyingine zilizotukuka pamoja na biashara yametoa mchango muhimu katika maendeleo ya Kenya.
  "Makampuni ya China yamekuwa yakifanya kazi nchini Kenya kwa miaka mingi na daima yanatoa mchango mkubwa kwa Kenya kupitia kuajiri wafanyakazi wa nchi hiyo na kuhamasisha jamii za wenyeji. Tunajivunia juhudi zao na tunatumaini wataweza kuendelea kusaidia jamii za wenyeji, " Balozi WU alisema.
  WU alibainisha kuwa mchango huo wa China unatoa ujumbe kabambe kwamba jamii ya China nchini Kenya imedhamiria na iko tayari kusimama pamoja na watu wa Kenya hata wakati wa matatizo.
  Huku akishukuru mchango kutoka China, Gavana wa Kaunti ya Pokot Magharibi John Lonyangapuo alitoa shukrani kwa serikali ya Rais Xi Jinping kwa kuonyesha urafiki wa kweli hasa katika wakati wa ugumu.
  "Kupitia mchango wenu, tumekuwa na uwezo wa kupunguza mateso yaliyowakumba watu wetu kutokana na janga hili". Gavana Lonyangapuo alisema katika barua yake ya kushukuru.
  Lakini hiyo haikutosha kwani wiki iliyopita mshauri na Naibu Mkuu wa misheni katika ubalozi wa China nchini Kenya Zhao Xiyuan baadaye alimkabidhi Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa hundi nyingine yenye thamani ya 100,000 dola za Marekani hili kusaidia mpango wa serikali wa kutoa msaada kwa familia zilizoathirika katika janga hilo.
  Ama kwa kweli, matendo haya yanathibitisha walivyonena wahenga kuwa "akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako