• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni toka China kuwasili Februari mwakani kusaka bidhaa za nyama na ngozi Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-12-23 09:50:03

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    KAMPUNI ya serikali ya China inayojishughulisha na bidhaa za Nyama na Ngozi inatarajia kuwasili nchini Tanzania mwezi February Mwakani ili kuangalia namna ya kukamata soko la bidhaa hizo nchini.

    Waziri wa Viwanda na biashara, Innocent Bashungwa alitaka wadau wa bidhaa hizo kujipanga kwa kuhakikisha wanaondoa changamoto zote kwani China kuna soko kubwa China ili ujumbe ukija Februari mwakani, wawe wamekaa vizuri.

    Waziri alisema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam alipokutana na wamiliki wa viwanda vya nyama, ngozi na wadau wengine wa sekta hiyo kujadili changamoto na mikakati mbalimbali inayowekwa na serikali ili kuiendeleza sekta hiyo.

    "Wakati tunatafuta soko la uhakika, wafugaji wafuge kwa tija, mifugo kidogo itoe mazao mengi kupitia mnyororo wa thamani. Tujipange vizuri maana kuna soko kubwa China ili ujumbe ukija Februari mwakani, tuwe tumekaa vizuri."anasema

    Waziri alibainisha kuwa, Tanzania ni ya pili kwa ufujaji barani Afrika ikiwa na ng'ombe milioni 32. 5 mbuzi milioni 20.5 na kondoo milioni 5.5.

    "Tanzania kuna viwanda tisa vya ngozi, lakini vinavyofanya kazi ni vitano, pia, upo uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha nyama Namanga mkoani Arusha na kingine cha nyama kilicho Morogoro na bahati nzuri, vyote vina uwezo mkubwa," alisema.

    Bashungwa ametaka wafugaji nchini kuongeza mnyororo thamani ya mifugo wao wakiwamo ng'ombe, badala ya kuridhika na mazao duni ya maziwa, ngozi na nyama pekee.

    "Tumezoea kwa mfano, katika ng'ombe tunapata maziwa, ng'ombe na ngozi, tusiridhike na hivyo tu, kuna mazao mengine ya kukuza uchumi wa wafugaji na taifa. Mnyororo wa thamani uliopo katika mifugo yetu ni mkubwa, lakini bado hatujanufaika ipasavyo,"alisema waziri.

    Alisema sekta hiyo ikiimarishwa, itaongeza ajira nchini na kukuza uchumi kwani inashangaza kuona licha ya serikali kutengeneza mazingira mazuri ya soko la ngozi ghafi nchini, bado jozi milioni 50 kati ya jozi milioni 55 zinazohitajika nchini, huagizwa kutoka nje ya nchi huku jozi milioni 1.2 pekee zikizalishwa nchini.

    Alisema Ngozi ghafi inayokwenda nje inatozwa asilimia 80 ili kuzuia kasi ya upelekaji nje na badala yake, ngozi iongezwe thamani nchini.

    Mmoja wa wadau wa sekta hivyo, Chrisant Mzindakaya alisema miongoni mwa njia za kuongeza tija katika ufugaji, ni Watanzania kuboresha (kunenepesha) mifugo ili kupata mazao bora ikiwamo nyama na pia, wazingatie suala la huduma na kwa mifugo.

    "Tusingoje kila kitu serikali ifanye, tunaweza kujiunga hata wafugaji watatu, wanne, watano wa maeneo jirani tukatengeneza josho, lazima tuwe wabunifu… kwa sasa hatufanyi vizuri katika soko kwa kuwa wengi wetu ni wachungaji si wafugaji," alisema Mzindakaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako