• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Tanzania na China yasaini mkataba kushirikiana kuondoa umasikini

  (GMT+08:00) 2019-12-30 10:21:23

  Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

  MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali saba kwa kila nchi kutoka Tanzania na China yamesaini mkataba wa ushirikiano katika nyanja tofauti kwa lengo la kuondoa umasikini.

  Hatua hiyo imefikiwa jana wakati wa uzinduzi wa mpango wa ujenzi wa Jumuiya ya njia ya hariri, mpango huo wa China unakuwa wa kwanza kuzinduliwa katika nchi za Afrika Mashariki na kusini na kusaidia katika usalama na amani, Ardhi, afya ya wanawake na watoto na mengineyo katika kuondoa umasikini.

  Katika uzinduzi huo ulihudhuriwa na naibu Spika wa China, Ji Bingxuan, Spika wa bunge la Tanzania, Job Ndugai, balozi wa Tanzania China Mbelwa Kairuki na wawakilishi wa asasi zilizosaini mkataba za China na Tanzania.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke alisema katika mkutano wa pili wa kimataifa wa ushirikiano wa njia moja ukanda mmoja uliofanyika April mwaka huu,mtandao wa taasisi zisizo za kiserikali China ulizindua mpango huo.

  Alisema lengo lake ni kutoa misaada kwa asasi za kiraia kutoka nchi za ukanda mmoja na njia moja kwa kufanya semina, kutembeleana na miradi ya kuboresha maisha jambi lililopata mrejesho chanya.

  Naye Spika Ndugai alisema ushirikiano huo ni wa pekee kwa imezoewa ule wa kiserikali, bunge au nyinginezo lakini kwa taasisi zisizo za kiserikali ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya Watanzania.

  Alisema baada ya Rais wa China Xi Jinping kusaidia fedha nyingi nchi za Afrika ili kuleta maendeleo hiyo ni fursa ya taasisi katika kuleta maendeleo ya wananchi.

  Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya kuluza uhusiano kati ya China na Tanzania (TCFPA) Dk Salim Ahmed Salim katika hotuba yake iliyosomwa na katibu wa taasisi hiyo, Joseph Kahama alisema taasisi hizo zimeungana katika kuondoa umasikini kwa kuhakikisha wanafuata sheria zinazosimamia asasi hizo.

  Pia kuheshimu mipaka ya nchi, bila kuingilia masuala ya ndani ya nchi husika pamoja na usawa na manufaa kwa wote.

  Alisema taasisi hiyo ya kuhamasisha mahusiano itahakikisha fedha zitakazotolewa zinafikia walengwa, kutoa ripoti serikalini huku wakihakikisga zinafanya kazi kwa matakwa ya kisheria.

  "Hakuna hofu katika utekelezaji wa makubaliano hayo yanayohamasisha muingiliano wa watu wa nchi hizi mbili kwani uzinduzi wake umeshuhudiwa na spika wa bunge china ambaye ni kiongozi mkubwa" Alisema.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako