• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Madaktari toka China watoa msaada wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 15 kwa Taasisi ya Moyo JKCI

  (GMT+08:00) 2019-12-30 16:37:32

  Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

  MADAKTARI toka china wanaofanya kazi nchini Tanzania wametoa msaada wa vifaa tiba na dawa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

  Mwakilishi wa Balozi wa Jamhuri ya watu wa China nchini Yuan Lin alisema msaada wa vifaa tiba pamoja na dawa walizozitoa katika kupitia madaktari wa Kichina wanaofanya kazi hapa nchini unathamani ya shilingi milioni 15.

  "Ninaamini msaada huu ambao ni moja ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya afya utasaidia katika matumizi ya kila siku ya Hospitali na utachangia katika kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa", alisema Lin.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi katika Taasisi hiyo Dk. Delilah Kimambo alisema uhusiano wa Taasisi hiyo na Serikali ya watu wa Jamhuri ya China ulianza miaka mingi iliyopita hata Jengo la Taasisi hiyo lilijengwa kwa msaada wa Serikali hiyo.

  Alisema Taasisi hiyo pia imekuwa ikipokea madaktari kutoka nchini China ambao wanatoa huduma za matibabu ya moyo pamoja na kufanya kambi maalum za matibabu ya moyo pia madaktari na wauguzi kutoka JKCI wanakwenda nchini humo kwa ajili ya kupata utaalamu zaidi wa magonjwa ya moyo.

  "Tunajivunia kuwepo kwa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo watatu katika Taasisi yetu ambao wametoka nchini China. Madaktari hawa wamekuwa msaada mkubwa kwetu na kwa wagonjwa tunaowatibu katika kutoa huduma za matibabu ya moyo ikiwemo upasuaji kwa watoto na watu wazima"Alisema.

  Ameeleza kuwa selikali ya Jamhuri ya watu wa China kila baada ya miaka miwili huwatuma madaktari kwa ajili ya kufanya kazi ya kutoa huduma ya matibabu hapa nchini ambapo kwa mwaka 2018 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iliwapokea madaktari bingwa wa moyo watatu kwaajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo.

  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Agnes Kuhenga alisema JKCI imetumia zaidi ya shilingi bilioni 1.2 kwa mwaka 2019 kwa ajili ya kulipa gharama za matibabu ya moyo kwa wagonjwa wanaotoka katika familia maskini na wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama hizo.

  Agnes ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha alisema asilimia 10 hadi 15 ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo hawana kadi za bima ya afya na hawana uwezo wa kulipia gharama za matibabu.

  Alishukuru China kwa misaada mbalimbali ya huduma za afya wanayoitoa katika Taasisi hiyo na kwa upande wa vifaa tiba pamoja na dawa walizozitoa alisema zitatumika kwa wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kuchangia gharama za matibabu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako