• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sayansi na teknolojia zachangia sana udhibiti wa virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-05-06 15:18:06


  Serikali ya Kenya inatumia simu za mikononi kuwafuatilia wagonjwa wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Corona. Ofisa mwandamizi wa nchi hiyo amesema ufuatiliaji wa simu za mikononi unaanza mara moja baada ya mtu kutambuliwa kuwa na hatari ya kuambukizwa na virusi vya Corona na unaendelea hadi hatari hii itakapoondolewa.
  Wengi kati ya wale wanaofuatiliwa kwa kutumia simu zao za mikononi ni wasafiri ambao walifika nchini humo mwezi uliopita kupitia uwanja wa ndege. Wakati walipofika nchini humo, walidaiwa kujaza fomu kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini humo.
  Ingawa hatua hii imeleta wasiwasi juu ya kuvamia faragha ya watu na usalama wa data, lakini maofisa wa serikali wanasema virusi vya Corona vinaleta hatari kubwa zaidi na inapaswa kupambana na virusi hivyo kwa njia zote. Hatua hizo vilevile zinatumiwa katika nchi nyingine mbalimbali katika kufuatilia mlipuko wa virusi hivyo, zikiwemo Israel, Singapore, Korea Kusini na China.
  Nchini China, serikali iliweka kamera za CCTV kwenye milango ya wale waliowekwa karantini kwa siku 14, ili kuhakikisha hawaondoki na kutoa tahadhari kwa wengine wavae barakoa. Nchini Singapore, serikali ilizudua mpango ambapo inatumia ishara za Bluetooth kwenye simu za mikononi, ambayo ina uwezo wa kufuatilia kama watu wenye virusi wamewasiliana na watu wengine.
  Huko Hongkong watu wanaowekwa karantini wanapaswa kuvaa vifaa ambavyo vinaunganishwa na simu ya mikononi ili kuonesha sehemu wanapokaa halisi kwa mamlaka ya huko. Serikali ya Korea Kusini inatumia shughuli za kadi za mikopo, data ya simu za mikononi na video ya CCTV kuunda mfumo wa kufuatilia maambukizi ya virusi hivyo. Hizi ni baadhi ya nchi chache zilizoweka mkazo katika upimaji mapema duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako