• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiwango cha talaka chaongezeka kwa kasi baada ya mlipuko wa virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-05-12 08:47:05


  Wakati hali ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona inapoelekea kuwa nzuri nchini China, mwezi Machi kiwango cha talaka nchini China kimeongezeka kwa kasi, huku matukio ya matumizi ya mabavu nyumbani yakiendelea kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

  Mwanzoni mwa mwezi Machi, idadi ya maombi ya talaka kwenye mji wa Xi'an mkoani Shanxi na mji wa Dazhou, mkoani Sichuan iliweka rekodi mpya, na kuleta kazi kubwa kwa idara zinazohusika. Katika mji wa Miluo, mkoani Hunan, wafanyakazi wanakosa hata muda wa kunywa maji kutokana na kushughulikia kiasi kikubwa cha maombi ya talaka.

  Mwanasheria wa kesi za talaka wa mji wa Shanghai Bw. Steve Lee amesema, tokea mji wa Shanghai ulipofunguliwa katikati ya mwezi Machi, idadi ya kesi anazoshughulikia imeongezeka kwa asilimia 25. Mlipuko wa virusi vya Corona uliwalazimisha wanandoa wengi kukaa nyumbani pamoja kwa miezi miwili, "Kadiri watu wanapokaa pamoja kwa muda mrefu zaidi, ndivyo wanavyokuwa na malalamiko mengi zaidi. Watu wanahitaji nafasi kubwa zaidi, ambayo si kama tu kwa wanandoa vilevile kwa kila mtu."

  Hivi sasa kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa watu waliozaliwa baada ya miaka 80 kutalikiana ikilinganishwa na wazazi wao, mwanasheria mwingine wa mji wa Shanghai Bw. Yang Shenli amesema, tangu hatua za kuwekwa karantini zianze kutekelezwe mjini Shanghai, ameshughulikia kesi nne za takala za wanandoa ambao walizaliwa baada ya mwaka 1985, na wawili kati yao walitalikiana kutokana na sababu kuwa "kukaa nyumbani kumeongeza mikwaruzano kati yao."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako