• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dunia inahitaji maelezo mengi kutoka kwa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-05-13 15:32:18


    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani, hadi tarehe 11 idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona nchini Marekani imezidi milioni 1.3 na watu wengine karibu elfu 80 wamefariki dunia kwa ugonjwa.

    Hata hivyo sio tu Marekani imeshindwa kabisa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona ndani ya nchi, bali pia imekuwa nchi inayosababisha maambukizi mengi kwa nchi nyingine duniani. Kwa mfano gazeti la National Post la Canada limeripoti kuwa takwimu zilizokusanywa katika majimbo manne yenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini humo zimeonesha kuwa maambukizi mengi yaliyotoka nje hayakutoka China, bali Marekani. Waziri mkuu wa Australia Bw. Scott Morrison hivi karibuni alisema kati ya maambukizi ya virusi vya Corona yaliyotoka nje ya Australia, mengi yalitoka Marekani, kauli ambayo ilizua mjadala mkubwa, na hata kuna mtu alisema kwa mujibu wa mantiki ya viongozi wa Marekani, hali hii inamaanisha kuwa virusi vya Corona vinaweza kuitwa "virusi vya Marekani"?

    Wakati huohuo watu wamegundua kuwa mwezi Julai mwaka jana, ugonjwa wenye dalili kama za nimonia usiojulikana kusababishwa na virusi gani uliibuka katika jimbo la Virginia, Marekani na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 50 kuumwa. Hapo baadaye, maabara ya kemikali na bailojia ya Fort Detrick iliyo katika jimbo jirani la Maryland ilifungwa kisirisiri. Vilevile, katika msimu wa mafua wa mwaka jana, watu milioni 26 waliumwa na wengine elfu 12 walifariki dunia, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko ile ya miaka ya nyuma…… Matukio hayo yaliyotajwa yanaonekana kama ni mambo yaliyotokea kwa bahati mbaya. Lakini Marekani inatakiwa kutoa maelezo kwa dunia nzima kuhusu maswali hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako