• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia 80 ya vijana waliozaliwa baada ya mwaka 1990 wana wasiwasi kuona matokeo ya upimaji wa hali ya afya

    (GMT+08:00) 2020-06-22 17:05:16


     Kupima hali ya afya kwa muda unaopangwa kunatakiwa kuwa tabia ya kawaida kwa watu wa hivi sasa. Lakini katika mahojiano yaliyofanyika hivi karibuni mitaani, asilimia 80 ya watu waliozaliwa baada ya mwaka 1990 wanasema wana wasiwasi ya kuona ripoti ya upimaji wa afya, kwani wengi kati yao wanakabiliwa na mashinikizo mbalimbali yakiwemo kununua nyumba, kutafuta kazi, kuchuma pesa na kutafuta wachumba, wanaogopa kugundua matatizo yao kiafya.

    Matokeo ya mahojiano yameonesha kuwa, watu wengi waliozaliwa baada ya mwaka 1990 wanafahamu umuhimu wa kujenga afya na upimaji wa afya, lakini pia hawana tahadhari za kutosha juu ya njia zisizo mwafaka za kuishi, na kuchukua msimamo wa kupuuza hatari zinazokabili afya, na kushindwa kukabiliana na matatizo yao ya kiafya.

    Kutokana na mahojiano hayo, mambo yanayotakiwa kuzingatiwa ni kuwa watu wengi wanachukua hali ya kuwa na nusu afya kuwa ni hali ya kawaida kwa watu wote, baadhi yao wanaona unene, na shinikizo la juu la damu si matatizo makubwa, wala hawaoni kuchelewa kulala na vichocheo vibaya vinaleta hatari kwa afya. Aidha, ingawa baadhi yao wanajua umuhimu wa mienendo mizuri ya \ya kuishi, lakini kutokana na shinikizo kubwa la kazi na maisha, wanashindwa kufuata mienendo miziri ya kuishi na kuleta matatizo mbalimbali ya kiafya.

    Hivi sasa, kulala vizuri na kula chakula salama yamekuwa mambo magumu yanayowakabili watu waliozaliwa baada ya mwaka 1990. Tabia ya kuishi kwa njia ya kiafya inatakiwa kujengwa wakati wa ujana, na kupima hali ya afya kwa muda uliopangwa na kuzingatia matokeo ya upimaji vinatakiwa kuwa mambo ya kisasa yanayofuatiliwa na vijana kwa hivi sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako