• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Je, ni kweli vipaji vya watoto vinaweza kupimwa kwa njia ya mate?

    (GMT+08:00) 2020-06-23 16:18:30


    Wazazi wote wana matumaini makubwa juu ya mustakabali wa watoto wao. Lakini ukiambiwa kama unaweza kujua vipaji vya watoto wako baada ya upimaji wa milimita kadhaa za mate, utaamini?

    Hivi sasa kuna aina nyingi za bidhaa za upimaji wa jeni wa watoto ili kupima vipaji vyao, na gharama zake si kubwa sana, mambo ya upimaji yanahusisha vipaji vya watoto katika kuchea, uchoraji, michezo au muziki. Upimaji wa aina huo unafanyika kwa kuchukua mate mdomoni, na matokeo yatapatikana ndani ya wiki moja hadi mwezi mmoja.

    Meneja wa kampuni moja ya upimaji wa jeni ya mji wa Chongqing ameeleza kuwa, mambo ya upimaji yanahusisha vipaji vyote vya watoto, mbali na vipaji vya kawaida vilivyotajwa hapo awali, pia yanahusisha uwezo wa uongozi, kukabiliana na shinikizo, kujifunza kutokana na uzoefu wa kushindwa…

    Lakini je, mambo haya kweli yanaaminika? Wataalamu wanaonavipaji hivyo vinavyotegemea jeni na molekuli tofauti vinatakiwa kupimwa baada ya kufanya utafiti juu ya idadi kubwa ya watoto. Lakini hadi sasa bado hakuna data za aina hiyo. Ndiyo maana kupima vipaji kwa kutumia jeni mbili tatu ni kama kupiga ramli, na haipaswi kuamini bidhaa za aina hii. Pia wataalamu wanapendekeza wazazi kuzingatia zaidi umuhimu wa mafunzo za nyumbani na shuleni kwa watoto, wala si kutegemea matokeo ya upimaji wa jeni wa watoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako