• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanamume agunduliwa kuambukizwa virusi vya Ukimwi baada ya kufunga ndoa

  (GMT+08:00) 2020-05-29 15:54:22


  Wachumba waliopanga kufunga ndoa walikwenda kufanyiwa upimaji wa afya. Muda mfupi baada ya kufunga ndoa, mwanamume huyo alikuwa na homa, na hali yake ya afya haikuwa nzuri, na alikwenda hospitalini na kugunduliwa na virusi vya Ukimwi. Mwanamume huyo hapendi kuvuta sigara, na hakuwahi kutoa damu, na mke wake ni mwenzi wake wa kipekee wa kimapenzi, hakujua hata kidogo jinsi alivyoambukizwa virusi vya Ukimwi.

  Baada ya hapo, mchumba wake alikiri kuwa yeye ana virusi vya Ukimwi. Hali hii ilimsikitisha sana mwanamume huyo. Lakini jambo linalombabaisha zaidi ni kuwa, tayari yeye na mke wake walishafanyiwa upimaji wa afya kabla ya kufunga ndoa, kwa nini hawakuambiwa hali hii.

  Kituo cha upimaji wa afya kinasema, hali hii imeshagunduliwa wakati walipofanyiwa upimaji, lakini kilimwarifu mke wake peke yake matokeo, ili kulinda usiri wa wagonjwa.

  Baada ya hapo, mwanamume huyo alitoa mashitaka kwa kituo hicho cha upimaji wa afya mahakamani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako