• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Je, ni wanaume au wanawake ambao ni rahisi zaidi kudanganywa kupitia mtandao wa Internet?

  (GMT+08:00) 2020-06-01 11:11:03


  Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya mtandao wa Internet, maisha ya watu yanategemea zaidi mtandao wa Internet. Wakati kuna watu wanaonufaika kutokana na mtandao huo, pia wapo wanaokabiliwa na hatari mbalimbali, ikiwemo udanganyifu kupitia mtandao wa Internet.

  Takwimu zilizotolewa na Kampuni ya Tencent mwaka 2019 zimeonesha kuwa, udanganyifu wa kibiashara, wa kufanya urafiki na kutoa nafasi za ajira ni aina tatu kubwa za udanganyifu kupitia mtandao wa Internet.

  Kati ya watu wenye umri wa miaka mbalimbali waliowahi kudanganywa, wale waliozaliwa baada ya mwaka 1990 ni wengi zaidi ambao wanachukua asilimia 48, na idadi ya wanaume ni mara 1.7 kuliko ile ya wanawake, lakini wastani wa kiasi cha fedha wa wanawake ni mara tatu kuliko wanaume. Kadiri umri wa miaka ya wanawake unavyozidi kuongezeka, ndivyo uwezekano wa kudanganywa unavyozidi kuongezeka. Hali ya wanaume kudanganywa ni tofauti na ile ya wanawake, uwezekano wa kudanganywa unazidi kupungua wakati umri wao unapoongezeka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako