• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapendekezo yanayofuatiliwa na watu wakati wa "Mikutano Miwili" ya China

    (GMT+08:00) 2020-05-25 16:19:59


    "Mikutano Miwili" ya China kwa mwaka huu inaendelea kufanyika hapa Beijing, na kuna mapendekezo mengi ambayo yanafuatiliwa sana na watu.

    1. Kwanza, mapendekezo yanayohusu kulinda wanyama pori yametolewa na wajumbe wengi wa Baraza la Mashauriano ya Kisasa la China CPPCC. Mjumbe Lv Hongbin, ambaye pia ni naibu mkuu wa shirikisho la wanasheria la China ametoa wito wa kukamilisha sheria ya makosa ya jinai ya kula wanyama pori. Amesema hivi sasa wanyama walioorodheshwa katika sheria hiyo ni wachache, ametaka orodha hiyo iongezewe, na wale watakaokula wanyama pori bila kujali sheria hiyo waadhibiwe kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai.

    2. halafu, kwa mujibu wa "kigezo cha kimsingi cha Benki ya mbegu za kiume za binadamu na kanuni za teknolojia", wanaume wote bila ya kujali kama wameoa au la, wanaweza kutoa ombi kuhifadhi mbegu zao kwa lengo kulinda afya ya kizazi au kufanya maandalizi kwa ajili ya mpango wa uzazi katika siku za baadaye. Lakini kwa wanawake ambao hawajaolewa, hawawezi kuhifadhi mayai kwa kutumia teknolojia. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, idadi kubwa ya wanawake wanabeba majukumu ya kazi na familia, na wengi wamepoteza muda bora wa uzazi. Kuna wengine ambao hawajaolewa na wanataka kuwa na mtoto, wanaweza kwenda nje ya nchi au mashirika yasiyo halali kutafuta njia ya kuhifadhi mayai yao. Kutokana na hali hii, mjumbe wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bibi Peng Jing ametoa pendekezo la kufanya marekebisho ya sheria, na kuwapa wanawake haki sawa ya uzazi.

    3. Pendekezo lingine linalofuatiliwa na watu lilitolewa na naibu profesa wa kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Shanghai Huang Qi, ambalo linasema wahalifu wa kijinsia wakirejea kwenye jamii baada ya vifungo, kuna haja kuwawekea mipaka ya kufanya kazi zinazohusiana na watu wasio wa wazima.

    4.Habari nyingine ya uhalifu iliyozusha mjadala mkubwa mwaka 2020, ni tukio la "mvulana mwenye umri wa miaka 13 kumwuua binamu yake mwenye umri wa miaka 10". Uhalifu kama huo unaofanywa na watu ambao bado si watu wazima ni tatizo kubwa linalokabili China na nchi nyingine duniani. Kiini cha suala hilo ni kama watoto wanaweza kuhukumiwa kama wakifanya uhalifu?

    Kwa mujibu wa sheria za sasa za China, watu wasiotimiza umri wa miaka 14 wakifanya uhalifu hawapaswi kubeba jukumu la kisheria, kutokana na hayo, mvulana huyo aliyemwua binamu yake hatahukumiwa. Lakini kimaadili hali hii haiwezi kukubaliwa. Ndiyo maana wajumbe wengi wametoa mapendekezo kuboresha vifungu vinavyohusika vya kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako