• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Suala la ubaguzi wa rangi nchini Marekani laweka vizuizi kwa mapambano dhidi ya virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-05-28 15:55:07


  Marekani ikiwa nchi yenye idadi kubwa ya wahamiaji, uhusiano kati ya watu wenye asili za nchi mbalimbali una utatanishi. Wakati mlipuko wa virusi vya Corona ukienea nchini humo, vitendo vya wanasiasa wa Marekani vimelifanya suala la ubaguzi wa rangi lipambe moto.

  Katika kipindi cha mwanzo cha mlipuko wa janga hili, baadhi ya wanasiasa wa Marekani na vyombo vya habari vilifanya mashambulizi yenye madhumuni mabaya dhidi ya makundi na nchi fulani, na kuzusha matukio mengi ya ubaguzi wa rangi: Mwanamke wenye asili ya Asia alimwagiwa asidi mjini New York, mwanafunzi wa sekondari mwenye asili ya Asia kwenye Jimbo la California alijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na kutibiwa hospitali, na watu watatu wa familia moja wa Jimbo la Texas walichomwa kwa kisu…

  Tovuti ya Time ya Marekani imeripoti kuwa, waathiriwa wa matukio yote 15 yanayohusiana na ubaguzi kutokana na janga la virusi vya Corona ni watu wenye asili ya Asia. Ripoti hii pia imekariri habari za kundi moja la ushawishi zikisema, tangu mlipuko wa virusi vya Corona, shirika hilo limepata ripoti kuhusu matukio 1,200 ya mashambulizi dhidi ya watu wenye asili ya Asia kote nchini Marekani.

  Hivi sasa ubaguzi wa rangi unaonekana katika kutokuwepo kwa usawa miongoni mwa watu wenye asili za nchi mbalimbali za kigeni nchini Marekani. Takwimu kutoka Ofisi ya mwendesha mashtaka ya Brooklyn mjini New York zimeonesha kuwa, kati ya tarehe 17 Machi hadi tarehe 4 Mei, miongoni mwa watu 40 waliokamatwa kutokana na kukiuka kanuni ya kuweka umbali unaopangwa na watu, 35 ni watu wenye asili ya kiafrika, wanne wenye asili wa Latin Amerika, na mwingine mmoja ni mzungu. Uchunguzi wa maoni ya raia uliofanywa na Gazeti la Washington Post umeonesha kuwa, kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, kiwango cha kupoteza ajira kwa watu wenye asili ya Latin Amerika na Afrika ni asilimia 20 na asilimia 16.Wakati huo huo, kiwango hicho kwa wazungu ni asilimia 11 tu. Jambo linalosikitisha ni kwamba, kutokana na ukosefu wa vifaa vya matibabu, watu wenye asili za nchi za kigeni walipuuzwa. Takwimu zilizotolewa katikati ya mwezi Aprili na Mfuko wa utafiti wa Ukimwi wa Marekani na Chuo cha afya ya umma cha Rollins kwenye Chuo Kikuu cha Emory zimeonesha hali duni ya wamarekani wenye asili ya kiafrika:

  Watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona na waliofariki kutokana na virusi hivyo wanachukua asilimia 52 na asilimia 58 mtawalia, kiwango ambacho kinazidi kwa kiasi kikubwa kuliko kiwango cha idadi yake kati ya idadi ya jumla ya watu nchini Marekani cha asilimia 13. Wanasayansi wa Chuo cha utafiti wa afya cha Marekani wamedokeza kuwa, mashirika ya matibabu ya Marekani yataacha kwanza matibabu kwa watu wenye asili ya kiafrika kutokana na ukosefu wa mashine ya kuwasaidia wagonjwa kupumua. Suala la ubaguzi wa rangi la Marekani limeweka vizuizi kwa mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako