• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni changamoto kubwa kwa nchi za Afrika Mashariki kutafuta uwiano kati ya uendeshaji wa uchumi na kinga na udhibiti wa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-05 18:46:11


    Hivi karibuni, baadhi ya nchi zimeanza kutekeleza hatua za kuondoa zuio baada ya hali ya maambukizi ya virusi vya Corona kuonesha mwelekeo mzuri, ili kuhimiza hatua ya kurejesha mambo ya uchumi na jamii. Nchini China, minyororo ya uzalishaji imerejeshwa kwa kiasi kikubwa, nchi za Ulaya zikiwemo Ujerumani, Uingereza na Ufaransa pia zimeanza kurejesha uzalishaji mali na masomo hatua kwa hatua. Nchi za Afrika zinazokabiliwa na matatizo ya afya na uchumi vilevile zina mahitaji ya haraka ya kurejeshwa kwa uchumi.

    Nchi za Afrika Mashariki haswa Tanzania na Uganda imepata hasara kubwa katika shughuli za utalii na hoteli, malaki ya watu wanakabiliwa na tishio la kupoteza ajira, mbali na hayo fedha za kigeni na mapato ya ushuru pia zimeathiriwa vibaya. Serikali ya Uganda ilitangaza kurejesha biashara katika hoteli na migahawa yote kuanzia tarehe 26 Mei, mawasiliano ya umma pia yatarejeshwa kuanzia tarehe 4 Juni. Rais John Magufuli wa Tanzania pia alitangaza kutoa kipaumbele kwa uchumi katika kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona, na kufungua tena anga ya Tanzania kwa ndege za kimataifa za abiria, na watalii wanaoingia nchini Tanzania kutokuwa na haja ya kuwekwa karantini kwa siku 14.

    Hatua hizo za kupunguza zuio za nchi za Afrika Mashariki zimeleta wasiwasi. Uchambuzi unaona kuwa janga la virusi vya Corona halitamalizika ndani ya muda mfupi, huku idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona ikizidi kuongezeka, hatua za kupunguza zuio zitaleta hatari na hasara isiyokadiriwa. Kwa hiyo kuna changamoto kubwa kwa nchi za Afrika Mashariki, katika kutafuta uwiano kati ya maendeleo ya uchumi na mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako