• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Basi moja mkoani Shandong latangaza mazoezi ya lugha ya kiingereza kwa wanafunzi ya muda wa mwaka mmoja

    (GMT+08:00) 2020-06-09 16:14:39


    Tarehe 27 video inayoonesha basi moja lililobeba wanafunzi wa sekondari No.7 ya mji wa Jinan wa mkoa wa Shandong likitangaza sauti ya mazoezi ya lugha ya kiingereza kwa wanafunzi hao, kufanya mazoezi ya kusikiliza wakiwa wamepanda basi, inafuatiliwa sana na watu.

    Watumiaji wa mtandao wa Internet wanasema, "Hakika itawasaidia wanafunzi!""Endeleeni na juhudi zenu!"

    Mfanyakazi wa Sekondari ya No.7 wa mji wa Jinan wa Mkoa wa Shandong ameeleza kuwa, ili kuwasaidia wanafunzi wa mwaka wa tatu wa sekondari ya juu wanaojiandaa kwa ajili ya mtihani wa kujiunga na vyuo vikuu ambao ni mtihani muhimu zaidi kwa wanafunzi wote, kuhakiki masomo yao na kuinua uwezo wao wa lugha ya kiingereza, baada ya kujadiliana na kampuni ya basi, waliamua kutangaza mazoezi ya lugha ya kiingereza kwenye basi hiyo, hadi mtihani mkuu utakapoanza. Mfanyakazi huyo alisema, wanafunzi wote wanafurahishwa na hatua hiyo, wakiona kuwa inawasaidia katika masomo yao ya kiingereza.

    Kwa mujibu wa mfanyakazi huyo, basi hilo namba S659 ni basi maalumu linalowabeba wanafunzi wa mwaka wa tatu wa sekondari hiyo, na limetangaza mazoezi ya masomo ya kiingereza kwa muda wa mwaka mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako