• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Familia mbili zagundua kuwa watoto wao walibadilishwa kwa makosa baada ya kufanyiwa upimaji wa damu na DNA

    (GMT+08:00) 2020-07-06 18:31:40


    Kama ukigundua kuwa mtoto wako si wako bila shaka utashangaa sana, si ndiyo? Lakini hivi karibuni jambo kama hilo limetokea.

    Mwezi Februari mwaka huu, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 28 kutoka mkoa wa Jiangxi anayeitwa Yao Ce aligunduliwa kupata saratani ya ini, wakati mama yake alipotaka kumwokoa kwa kumchangia ini lake, upimaji wa damu na wa DNA ulionesha kuwa Yao Ce si mtoto wake wa damu. Baada ya kufanyika kwa uchunguzi, walifahamu kuwa ni kosa la hospitali lililowafanya watoto wabadilishwe kwa makosa wakati walipozaliwa miaka 28 iliyopita, hali ambayo ilimfanya Yao Ce kukosa fursa ya kupata chanjo ya Hepatitis B, na kukumbwa na ugonjwa unaoweza kuepukika.

    Tarehe 15 Juni mwaka 1992, wajawazito wawili Xu Min na Du Xinzhi walijifungua kwenye Hospitali ya pili ya mji wa Kaifeng ya Mkoa wa Henan, watoto wao walibadilishwa kwa makosa baada ya kuzaliwa. Tarehe 30 Aprili familia hizo mbili zilikutana katika mji wa Jiujiang mkoani Jiangxi, lakini bado hazijafikia makubaliano na hospitali kuhusu fidia.

    Hivi sasa wazazi wa Yao Ce wanatumai mama yake halisi ataweza kumwokoa mtoto wake, lakini jambo linalosikitisha ni kwamba, mama yake halisi Du Xinzhi pia ana saratani ya ini na amefanyiwa upasuaji, na sasa anapatiwa tibakemikali.

    Makosa kama hayo ya kubadilisha watoto kwa makosa si kama tu yanaziletea uchungu familia, bali pia yanaleta uchungu usioweza kuondolewa kwa watoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako