• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Unachukua maoni gani juu ya makosa aliyoyafanya nyota?

    (GMT+08:00) 2020-06-12 15:33:13


    Hivi karibuni nyota mmoja wa China Luo Zhixiang amekuwa anafuatiliwa sana na watu. Nyota huyo anajulikana kwa uimbaji, kucheza dansi na uigizaji kwenye filamu, na kufurahisha sana watu. Lakini mwezi Aprili mchumba wake aliyeishi pamoja naye kwa miaka tisa, alitoa tangazo la kuachana naye kutokana na Bw. Luo Zhixiang kumsaliiti mara kwa mara katika uhusiano huo, na kudokeza mambo mengi halisi ambayo yaliwastaajabisha sana watu, hali ambayo iliathiri vibaya kazi za nyota huyo hapa China bara, na kumlazimisha arudi mkoani Taiwan.

    Hata hivyo kazi zake mkoani Taiwan pia zimeathiribiwa. Vyombo vya habari vya mkoa wa Taiwan vimeripoti kuwa, thamani ya duka lake la nguo l mkoani humo imepshuka kwa zaidi ya nusu kuliko zamani. Mbali na hayo, watumiaji wengi wa mtandao wa Internet wameeleza kuwa hawataunga mkono muziki zake na pia hawatanunua bidhaa yoyote inayohusiana naye.

    Ni kwa nini matatizo hayo yanamkabili? Ni kwanini watu wamekuwa na msimamo mkali dhidi yake? Akiwa ni mtu maarufu kwa miaka mingi, anatakiwa kujua maana ya maadili na wajibu wake kwa jamii. Kama yeye hawezi kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana, basi ni suala la wakati tu kwa yeye kuondolewa jukwaani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako