• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti unaonesha kuwa kama uzito wa mtu ukiongezeka kwa kilo tano, kiwango cha kufariki kinaongezeka kwa asilimia 11

    (GMT+08:00) 2020-06-17 12:54:19


    "Unene unaathiri vibaya vitu vyote." Hii si kauli ya kuchekesha. Uchunguzi uliofanywa na Jarida la Lishe la Ulaya na Jarida la Taasisi ya Matibabu ya Marekani umethibitisha madhara mapya ya unene.

    Utafiti uliofanywa na Jarida la Lishe la Ulaya uliowahusisha watu milioni 1.09, umeonesha kuwa watu wazima wakiwa na ongezeko la uzito wa kilo 5, kiwango cha uwezekano wa kufariki kinaongezeka kwa asilimia 11. Utafiti mwingine uliofanywa na Jarida la Taasisi ya Matibabu ya Marekani pia umethibitisha baada ya kuwachunguza wanawake 48,377 na wanaume 35,989, kuwa tangu watu wanapokuwa watu wazima hadi wakiwa na umri wa makamo, kila baada ya uzito wao kuongezeka kwa kilo 5, kiwango cha kufariki kwa wanaume na wanawake kinaongezeka kwa asilimia 9 na 14 mtawalia.

    Kituo cha saratani cha Ingram kimeshirikiana na watafiti wa Taasisi ya utafiti wa saratani cha Shanghai, kufanya utafiti kwa wachina zaidi ya elfu 80 na kugundua kuwa, kati ya wanawake wenye umri wa makamo ambao kiwango cha BMI kimezidi 23, kila baada ya uzito wao kuongezeka kwa kilo 5, kiwango cha kufariki kinaongezeka kwa asilimia 14, na kiwango cha kufariki kutokana na magonjwa ya mishipa ya damu kinaongezeka kwa asilimia 23. Hali ya wanaume inafanana na ile ya wanawake.

    Watafiti pia wamegundua kuwa japokuwa kiwango cha BMI hakizidi 23, ongezeko la uzito wa watu linaweza kuhusiana na aina nyingi za magonjwa sugu, ambayo inamaanisha kuwa watu wanatakiwa kudhibiti uzito wao tangu wanapokuwa na umri wa miaka 20, na baada ya kuwa na umri wa makamo, kila baada ya uzito wao kuongezeka kwa kilo 5, kiwango cha kufariki wanapokuwa wazee kinaongezeka kwa asilimia 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako