• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huduma ya kutambua rekodi ya ukatili majumbani kabla ya ndoa yazinduliwa Yiwu

    (GMT+08:00) 2020-07-15 10:43:56


    Juni 22, kamati ya siasa na sheria iliyo chini ya Kamati ya chama cha kikomunisti ya mji wa Yiwu mkoani Zhejiang, mahakama, chama cha wanawake, idara ya polisi, idara ya mambo ya kiraia na kituo cha usimamizi wa data mjini humo, wametangaza kuanzisha mfumo wa kukagua rekodi ya ukatili wa majumbani kabla ya kuandikisha ndoa, ambao utaanza kutekelezwa rasmi Julai mosi. Mfumo huu ni wa kwanza wa aina yake nchini China.

    Naibu mwenyekiti wa chama cha wanawake cha mji wa Yiwu Bi. Zhou Danying, amesema zamani watu waliweza tu kujua kama mwanandoa mwingine alikuwa na rekodi ya vitendo vya ukatili majumbani baada ya kufunga ndoa. Lakini sasa mfumo huu mpya unawawezesha watu wanaotaka kufunga ndoa kutambua kama upande mwingine ulikuwa na rekodi ya ukatili wa majumbani au la, kabla ya kufanya uamuzi wa kufunga ndoa, ili kuzuia na kupunguza ukatili wa majumbani.

    Ofisa huyo amesema ili kulinda faragha ya raia, mtu yeyote anayetaka kutumia huduma hiyo anatakiwa kuandikishwa kwa kutumia kitambulisho cha taifa, kutoa barua ya ombi kwa ofisi ya usajili wa ndoa na kusaini makubaliano kuhusu ulinzi wa faragha, kabla ya kupewa idhini ya kutumia mfumo huo.

    Imefahamika kuwa mahakama na idara za polisi mjini Yiwu zitawasilisha moja kwa moja rekodi ya watu waliohusika na ukatili wa majumbani kwenye kituo cha usimamizi wa data, ili kuhakikisha rekodi zote zinahifadhiwa kwa usahihi, na faragha za wanaohusika zinalindwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako