• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watumiaji wakubwa wa dawa za kulevya

    (GMT+08:00) 2020-07-03 16:23:50


    Hivi karibuni, habari kuhusu nyota mmoja Bibi Niu Mengmeng kukamatwa kutokana na kutumia dawa za kulevya imezusha mjadala mkubwa kwenye mtandao wa Internet.

    Habari kuhusu kukamatwa kwa Niu Mengmeng ilitangazwa tarehe 24 mwezi Mei, lakini yeye alikataa habari hii na kudai kuwa hakutumia dawa za kulevya na huo ulikuwa ni uvumi tu. Lakini baadaye idara ya polisi ilithibitisha kweli Bi Niu Mengmeng alijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na watu wengine, lakini kutokana na kuwa alichukua msimamo mzuri wa kujikosoa, na kukubali kuadhibiwa na kushiriki kwenye shughuli za kuachana na uraibu wa dawa za kulevya.

    Baada ya hapo watumiaji wa mtandao wa Internet wamekuwa na maoni tofauti kuhusu jambo hilo, baadhi wanaona Niu Mengmeng akiwa mtu anayejulikana nchini, kutangazwa mara kwa mara kwake kutumia dawa za kulevya kumeathiri heshima yake akiwa nyota, na pia kumeleta athari mbaya kwa vijana.

    Wengine wanaona kuwa hivi sasa nyota wengi wanajitangaza kwa habari mbalimbali zikiwemo habari mbaya, ikiwemo kutumia dawa za kulevya, ili kupata kiki. Pia kuna watu wasemao baadhi ya nyota wanatumia dawa za kulevya kutokana na shinikizo kubwa, na kama hawaathiri watu wengine, basi ni jambo linaloweza kueleweka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako