• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni shughuli ya kutoa msaada au kuvutia macho ya watu?

    (GMT+08:00) 2020-07-07 16:16:53


    Siku hizi, habari moja kuhusu "Mhalifu wa kudhalilisha watoto wa kike aliyeachiwa huru amepata msaada" imefuatiliwa na watu.

    Video imeonesha kuwa mwanamume Meng aliyeachiwa huru baada ya kuhukumiwa jela miaka minne kutokana na uhalifu wa kuwadhalilisha watoto wa kike, alishiriki kwenye shughuli la kumkaribisha lililoandaliwa na Shirika la utoaji wa ufadhili wa Mji wa Nanning, mkoani Guangxi. Mwanamume Meng alikuwa akicheza dansi kwenye shughuli hiyo ambayo ilitangazwa kama mkutano na waandishi wa habari.

    Bw Meng mwenye urefu wa mita 1.52 alizaliwa mjini Nanning, mkoani Guangxi, alijulikana kupitia mtandao wa Internet kutokana na mavazi yake na tabia yake zisizo za kawaida. Aliwahi kualikwa kufanya maonesho ya kuimba na kucheza dansi wakati duka moja la kuuza supu ya soya lilipofunguliwa, na kuitwa "mwana mfalme wa supu ya soya".

    Mwezi Agosti mwaka 2016, mwanamume huyo alimdhalilisha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita tu na kukamatwa na polisi. Baada ya hapo alikiri kufanya vitendo kama hivyo mara nyingi kati ya mwezi Julai hadi Agosti na kuhukumiwa kifungo cha miaka minne.

    Tarehe 8 Juni, Shirika la watu wa kutoa misaada kwa hiari liliandaa shughuli za kumkaribisha nyumbani. Mwanachama mmoja wa shirika la utoaji wa misaada kwa hiari la huko alisema, alipata taarifa kutoka kwa waandaaji wa shughuli hiyo ya kushiriki kwenye mkutano na waandishi wa habari, na kwamba kwenye mkutano huo mwanamume huyo hakuomba radhi kwa waathirika, alichofanya ni kuomba watu kuendelea kumwunga mkono.

    Watu wana wasiwasi juu ya shughuli hiyo, wakisema uhalifu wa mwanamume huyo unatofautiana na wizi na uporaji ambao unawaletea watu hasara ya kiuchumi tu, na katika baadhi ya nchi watu wanaowafanyia udhalilishaji watoto wa kike wanapaswa kufungwa maisha. Lengo la shirikisho hilo la kuandaa shughuli hii ni kujitangaza kutokana na kujulikana kwa mwanamume huyo au lina dhamira nyingine?

    Naibu mkurugenzi wa shirikisho hilo Bw. Zhang Yongjun alipofanyiwa mahojiano alisema, hatua hii ni kumwelekeza Bw. Meng arejee kwenye jamii, na kwamba sheria imemwadhibu kwa haki, kwanini watu hawataki kumsaidia? "

    Tarehe 9 Juni, Shirikisho la vijana wa kujitolea la mji wa Nanning lilitoa taarifa likisema halikuandaa shughuli yoyote ya kumkaribisha Bw. Meng kurejea kwenye jamii, watu au mashirika yanayofanya shughuli kama hii kwa kutumia jina la shirika hilo wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako