• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni kweli Wanawake wenye vyeo, Madaraka hawafai kuolewa?

    (GMT+08:00) 2020-07-08 15:36:09


    Kumekuwa na kasumba ambayo tayari imeshajengeka kwenye vichwa vya watu wengi hususan wanaume. Wanaamini kwamba, wanawake wakishakuwa na pesa au cheo fulani huwa ni vigumu sana kuolewa. Kwamba hawawezi kudhibitiwa na wanaume wao kwani nao wanajiona kwamba wana mamlaka kamili, hawawezi kutikiswa na wanaume.

    Mwanamke ana kazi nzuri, ana mshahara wake mzuri pengine kupita hata wa mwanaume, utamwambia nini? Anataka na yeye anyenyekewe na mume au mwanaume wake kama ambavyo vijana wa kiume wanavyomnyenyekea anapokuwa kazini au kwenye biashara yake.

    Ni vizuri sana kujifunza kwa undani ni nini hasa kinachosababisha haya? Ni hulka tu ya mtu ambayo wakati mwingine inaletwa na madaraka au pesa. Tabia zinazoletwa na pesa au madaraka, huwa ni vigumu sana kuzidhibiti, si wanawake tu hata wanaume wapo wanaoshindwa kujizuia. Wakipata vyeo au madaraka, hujikuta wamebadilika sana. Wanafanya mambo ya ovyo ambayo awali walikuwa hawayafanyi.

    Hivyo muhimu ni kujifunza tu kwamba, binadamu tunapaswa kuishi kama binadamu. Uwe na madaraka au hauna, utu uwe ndiyo kila kitu. Kiburi cha pesa au madaraka ni cha muda tu na kinaweza kutoweka muda wowote.

    Muhimu sana ni kuishi kwenye misingi ya kibinadamu. Kujiheshimu na kuheshimu wengine. Kujua nini wajibu wa mke au mwanamke kwa mwanaume wake au kujua nini wajibu wa mwanamme au mume kwa mke wake. Pesa na madaraka visikutoe akili ukafanya ya kijinga. Vitu vyote hivyo vinakuja, vinatafutwa na vinaweza kutoweka, lakini heshima na utu wako utabakia.

    Kwa msingi huo, wanawake wenye vyeo na madaraka wanaweza kuolewa na kuishi kwa nidhamu ya kike kama tu watazingatia yote haya. Kama tu hawataamua kujitoa ufahamu au kupofushwa na vyeo au madaraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako