• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni yawaajiri wanene kujaribu huduma ya kuwasaidia kupunguza uzito

    (GMT+08:00) 2020-07-16 10:30:00


    Kampuni moja ya mji wa Chongqing, China imeweka tangazo mtandaoni la kutafuta watu watano wenye uzito mkubwa kujaribu huduma yake ya kusaidia kupunguza uzito. Kazi hiyo ni ya muda wa miezi mitatu, mshahara wa msingi ni yuan elfu kumi kwa mwezi. Kama waajiriwa hao wakifanikiwa kupunguza uzito wao ndani ya muda huo, watapewa bonasi ya yuan moja kwa kila gramu iliyopungua.

    Mara baada ya kutolewa mtandaoni, tangazo hilo limevutia ufuatiliaji mkubwa katika mitandao ya kijamii. Baadhi ya wanamtandao wameandika ujumbe chini ya tangazo hilo kwamba "wataweza kupunguza uzito kwa kiasi kitakachofilisi kampuni hii."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako