• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanamke kutoka kijiji aibiwa nafasi ya kusoma Chuo Kikuu na mtu mwingine

    (GMT+08:00) 2020-07-20 15:49:58


    Mtihani wa kujiunga Chuo Kikuu ni mtihani muhimu kwa wanafunzi wengi, na mtihani huu huamua mustakbali wa maisha ya watu wengi. Kuna msemo usemao " Elimu huabadilisha maisha ya watu", hili pia ndio ambalo mwanamke kutoka kijiji mkoani Shandong Chen Chunxiu aliamini, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba, maisha yake yaliliiwa na na mtu mwingine kwa yuan elfu mbili.

    Hivi karibuni habari kuhusu mwanamke kuibiwa nafasi ya Chuo Kikuu na mtu mwingine" imekuwa inafuatiliwa sana na watu. Mwaka 2004, mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 20 hakupata barua ya kuitwa chuo kikuu baada ya kumaliza mtihani. Kwa hiyo alijiona kuwa alishindwa mtihani na kuamua kuondoka nyumbani kwenda kutafuta kazi. Alifanya kazi kwenye kiwanda cha kielektroniki, migahawa, na sasa yeye ni mwalimu wa shule ya chekechea. Aliendelea kufanya hivi hadi siku moja alipojiandaa kujiandikisha Chuo Kikuu kwa watu wazima, lakini ghafla aligundua kwenye tovuti kuwa alichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Ufundi cha mkoa wa Shandong miaka 16 iliyopita, na kumaliza masomo yake kwenye chuo kikuu hicho. Baada ya kuuliza idara zinazohusika ndipo alitambua kuwa nafasi yake iliibwa na mtu mwingine. Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa baada yaa uchunguzi, mwanamke aliyeiba nafasi hiyo anaitwa Chen Yanping, alichukua nafasi ya Chen Chunxiu kumaliza masomo ya chuo kikuu na kufanya kazi ya uhasibu kwa jina feki Chen Chunxiu. Baada ya kuripotiwa kwa habari hii, Chen Yanping alitambua kuwa alichukua nafasi ya Chen Chunxiu kusoma kwenye chuo kikuu, na kwamba ni shangazi yake ambaye amefariki ndiye aliyeshughulikia jambo hilo kwa kupitia mtu mwingine.

    Chuo Kikuu cha Ufundi cha mkoa wa Shandong kimekiri kuwepo kwa dosari kwenye hatua ya kukagua na kuthibitisha wasifu wa watu wanaowaandikisha. Hivi sasa Chen Yanping amesimamishwa kazi. Sasa Chen Chunxiu anataka kurejesha nafasi yake ya kujiunga chuo kikuu, na kutimiza ndoto yake ya kusomea chuo kikuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako