• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu ajiua baada ya kunyimwa fursa ya kuendelea na mtihani kutokana na kufanya udanganyifu

    (GMT+08:00) 2020-07-20 15:41:35


    Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Zhong Bei cha mkoa wa Shanxi alijiua baada ya kunyimwa fursa ya kushiriki kwenye mtihani kutokana na kufanya udanganyifu.

    Hii ni mara ya pili kwa mwanafunzi huyo kushiriki kwenye mtihani huu baada ya kushindwa mara ya kwanza, lakini alifanya udanganyifu wakati wa mtihani na kunyimwa fursa ya kuendelea na mtihani. Baada ya hapo, alitoka darasa na kujiua kwa kujirusha kutoka ghorofani Wazazi wa mwalimu huyo walisema, kifo cha mtoto wao kinatokana na mwalimu aliyesimamia mtihani kutomwonea huruma, na wanaona chuo kikuu kinapaswa kuwajibika.

    Baada ya tukio hilo, Chuo Kikuu cha Zhong Bei kilitoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii kuwa, video ya darasa na mashuhuda wote wamethibitisha kuwa mwalimu na mwanafunzi huyo hawakugombana. Idara ya usalama ya huko imeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo. Hivi sasa chuo hicho kinafanya mawasiliano na jamaa wa mwanafunzi huyo ili kushughulikia ipasavyo tukio hilo.

    Mkuu wa chuo hicho Bw. Shen Xingquan alisema, chuo kimethibitisha kuwa mwanafunzi huyo alifanya udanganyifu. Na wakati wa mtihani hakukuwa na uwezekano wa mwalimu kuonyesha huruma. Anaona kuwa mwalimu hakuchukua hatua zisizo mwafaka, na mwanafunzi huyo angeweza kusamehewa kama angeomba radhi na kufanya vizuri katika siku za baadaye. Pia amesema elimu haiwezi kuhakikisha wanafunzi wanaepukana tatizo la kisaikolojia. Wanafunzi wa vyuo vikuu ni watu wazima, na wanatakiwa kujua kuwa uaminifu unahusishwa kwenye sheria na kanuni za nchi, na kwamba Chuo Kikuu cha Zhong Bei kitaendelea kufuata kanuni kwa makini dhidi ya udanganyifu wakati wa mtihani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako