• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijana anayejuta kuuza figo yake aita polisi kuwakamata wafayabiashara wahalifu

    (GMT+08:00) 2020-07-22 20:54:17


    Kijana anayeitwa Xiao Ding aliyeishi kwenye maisha duni, aliuza figo yake kwa yuan elfu 55, sawa na dola za kimarekani elfu nane. Lakini baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa figo, alijuta na kuamua kuwaita polisi.

    Upasuaji huu ulifanyika kwenye chumba kimoja kilichoko kwenye makazi ya watu. Mara baada ya kumalizika kwa upasuaji, Xiao Ding alianza kuumwa sana, na kuona pesa alizopata ni chache sana. Hivyo aliwapigia simu polisi na kuwaambia jambo hili.

    Kutokana na maelezo ya Xiao Ding, polisi wamekamata kundi lenye zaidi ya watu kumi ambao wana kazi tofauti za kufanya upasuaji, kutafuta watu wanaouza figo na wale wanaotaka kununua figo kupitia mtandao wa kijamii.

    Kundi hilo limeuza mara mbili viungo vya binadamu. Upasuaji wa Xiao Ding ulifanikiwa, lakini mwingine ulishindwa, mtu aliyetaka kuuza figo alijiandaa kufanyiwa upasuaji kwenye hospitali moja mkoani Shanxi, lakini upasuaji ulifutwa kutokana na kutokuwa na dawa za ganzi.

    Kesi hiyo itasikilizwa na mahakama ya mji wa Taiyuan ya mkoa wa Shanxi.

    Katika miaka mingi iliyopita nchini China wagonjwa wengi wanakabiliwa na ukosefu wa viungo wananyohitaji haswa figo. Hivyo biashara haramu za viungo zimeibuka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako