• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sherehe ya kuhitimu kupitia mtandao wa Internet ni mwelekeo mpya kwenye vyuo vikuu vya China

    (GMT+08:00) 2020-07-22 19:01:03


    Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Hefei alihudhuria sherehe yake ya kuhitimu kupitia mtandao wa Internet nyumbani. Kwenye sherehe hiyo, wahitimu zaidi ya 400 na walimu wachache walijumuika wakiwa wamevaa barakoa, na zaidi ya wanafunzi 9,600 walikuwepo kwenye mtandao wa Internet.

    Wu alisema ni inafurahisha kwa yeye kushiriki kwenye sherehe hiyo chuoni, mtandao wa Internet unawaruhusu kupata uzoefu kama huu nyumbani, na kubadilishana uzoefu huo kupitia mtandao wa Internet, ambayo pia ni njia bora wakati wa kukabiliwa na janga la virusi vya Corona.

    Kwa kweli Wu ni mmoja kati ya wanafunzi milioni 8.74 nchini China wanaotarajiwa kuhitimu kutoka Chuo Kikuu mwaka huu. Kutokana na COVID-19, vyuo vikuu vingi vinaandaa sherehe kama hii kupitia mtandao wa Internet ili kuondoa majuto ya wanafunzi hao.

    Utafiti uliofanyika hivi karibuni na Gazeti la vijana la China umeonesha kuwa, wakati wa mlipuko wa COVID-19, asilimia 88.6 ya wahitimu wapya wa Chuo Kikuu cha China walisherehekea kuhitimu kwa njia ya mtandao wa Internet. Walitengeneza video za kuhitimu au kutazama sherehe za kuhitimu.

    Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Hefei Liang Liang amesema, katika miezi kadhaa iliyopita, wamehamishia masomo, taratibu za kuwaajiri walimu na hafla za kuhitimu kwenye mtandao wa Internet. Hizi ni hatua maalumu zilizochukuliwa katika kipindi hiki maalumu, na kwamba wanalotaka ni kuleta matokeo mazuri kwa maisha ya vyuo vikuu kwa wahitimu kwa njia zenye kiuvumbuzi kama hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako