• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing yafungua barabara zaidi kupima magari yanayojiendesha

    (GMT+08:00) 2020-07-21 15:48:16


    Beijing imefungua barabara nyingine 52 katika wilaya ya Haidian, kwa ajili ya upimaji wa magari yanayojiendesha, ili kuendeleza teknolojia ya kujiendesha.

    Kwa mujibu wa serikali ya wilaya ya Haidian, barabara hizo zenye urefu wa jumla wa kilomita 215.3, ziko kaskazini mwa mtaa wa Zhongguancun unaojulikana kutokana na kuwepo kwa makampuni mengi ya teknolojia ya juu, na ni sehemu ya eneo la vielelezo la teknolojia ya magari yanayojiendesha.

    Kulingana na mpango kazi, wilaya ya Haidian itaendelea kufungua barabara zaidi za kupima magari yanayojiendesha hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

    Katika siku zijazo eneo la vielelezo la teknolojia ya magari yanayojiendesha litaanzisha miradi mipya ya miundombinu inayojumuisha teknolojia ya kujiendesha, ramani zenye usahihi zaidi na akili bandia ya mawasiliano ya barabara.

    Mwezi Machi mwaka 2018, Beijing ilifungua barabara 33 zenye urefu wa jumla ya kilomita 105 kwa ajili ya kupima magari yanayojiendesha katika wilaya za Daxing, Shunyi na Haidian, ambazo zote ziko mbali na maeneo yenye watu wengi. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, Beijing ilikuwa imefungua barabara 151 zenye urefu wa kilomita 503.68 kwa ajili ya upimaji wa magari yanayojiendesha. Kulingana na mpango wa serikali ya Beijing, hadi kufikia mwaka 2022, barabara zenye urefu wa kilomita 2,000 zitafunguliwa kwa ajili ya majaribio ya magari yanayojiendesha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako