• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ni suala kubwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kusoma kwa muda usiotimia nusu saa kila siku

    (GMT+08:00) 2020-07-10 15:55:49


    Wanafunzi husoma vitabu kila siku kwa muda gani? Wanapenda kusoma vitabu gani? Hivi karibuni utafiti uliofanywa kwa wanafunzi 864 wa vyuo vikuu umeonesha kuwa, asilimia 50 ya wanafunzi wanasoma vitabu kwa muda usiotimia nusu saa, na zaidi ya asilimia 40 ya wanafunzi hawasomi kitabu hata kimoja kwa mwezi. Asilimia 60 ya wanafunzi hawaridhiki na hali ya ya usomaji.

    Katika zama ambayo mtandao wa internet ulikuwa haujaenea, maktaba ilikuwa ani sehemu iliyowafurahisha zaidi wanafunzi wa chuo kikuu, baadhi ya wanafunzi walipenda kusoma kwenye maktaba kwa siku nzima, hata hawakutaka kuondoka wakati muda wa kufunga ulipofika. Kusoma ni njia nzuri kunawaelimisha wanafunzi na kuongeza uwezo wao, lakini ni kwa nini kwa sasa idadi kubwa ya wanafunzi hawapendi kusoma?

    Baadhi ya watu wanaona kuwa, hali hii inatokana na wanafunzi wengi wamezoea mtandao wa internet. Chuo Kikuu cha Maryland cha Marekani kiliwahi kufanya uchunguzi kwa wanafunzi elfu moja. Wanafunzi hao hawakuruhusiwa kutumia chombo chochote ikiwemo simu ya mkononi ndani ya siku moja. Matokeo yameonesha kuwa, zaidi ya asilimia 90 ya watu walionesha wasiwasi baada ya kuacha simu ya mkononi.

    Njia zenye ufanisi za kuongeza muda wa kusoma na kupunguza kutegemea simu za mkononi na mtandao wa Internet ni kuongeza uwezo wa kujidhibiti. Wanafunzi wakipenda kutumia muda zaidi katika kusoma, watapata faida zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako